Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Mwanzo 14:22 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

22 Abramu akamwambia mfalme wa Sodoma, Nimeinua mkono wangu kwa BWANA, Mungu Aliye Juu sana, Muumba mbingu na nchi,

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

22 Lakini Abramu akamwambia mfalme wa Sodoma, “Naapa kwa Mwenyezi-Mungu, Mungu Mkuu, aliyeumba mbingu na dunia,

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

22 Lakini Abramu akamwambia mfalme wa Sodoma, “Naapa kwa Mwenyezi-Mungu, Mungu Mkuu, aliyeumba mbingu na dunia,

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

22 Lakini Abramu akamwambia mfalme wa Sodoma, “Naapa kwa Mwenyezi-Mungu, Mungu Mkuu, aliyeumba mbingu na dunia,

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

22 Lakini Abramu akamwambia mfalme wa Sodoma, “Nimeinua mkono wangu kwa Mwenyezi Mungu, Mungu Aliye Juu Sana, Muumba wa mbingu na dunia, na nimeapa

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

22 Lakini Abramu akamwambia mfalme wa Sodoma, “Nimeinua mkono wangu kwa bwana, Mungu Aliye Juu Sana, Muumba wa mbingu na dunia, na nimeapa

Tazama sura Nakili




Mwanzo 14:22
22 Marejeleo ya Msalaba  

Mfalme wa Sodoma akamwambia Abramu, Nipe mimi hao watu, na hizo mali uchukue wewe.


Abramu alipokuwa mtu wa miaka tisini na tisa, BWANA akamtokea Abramu, akamwambia, Mimi ni Mungu Mwenyezi, uende mbele yangu, ukawe mkamilifu.


Abrahamu akapanda mkwaju huko Beer-sheba, akaliitia huko jina la BWANA Mungu wa milele.


nami nitakuapisha kwa BWANA, Mungu wa mbingu, na Mungu wa nchi, kwamba hutamtwalia mwanangu mke katika binti za Wakanaani ambao nakaa kati yao;


Basi Daudi akatuma wajumbe kwa watu wa Yabesh-gileadi, na kuwaambia, Na mbarikiwe ninyi na BWANA, kwa kuwa mmemtendea bwana wenu fadhili hii, yaani Sauli, mkamzika.


Lakini akasema, Kama BWANA aishivyo, ambaye nimesimama mbele yake, sipokei kitu. Akamshurutisha apokee; lakini akakataa.


Ee BWANA, ukuu ni wako, na uweza, na utukufu, na ushindi, na enzi; maana vitu vyote vilivyo mbinguni na duniani ni vyako; ufalme ni wako, Ee BWANA, nawe umetukuzwa, u mkuu juu ya vitu vyote.


Uniponye, unitoe, Katika mkono wa wageni. Vinywa vyao vyasema visivyofaa, Na mkono wao wa kulia ni mkono wa uongo.


Vinywa vyao vinasema visivyofaa, Na ambao mikono yao ya kulia ni ya uongo.


Nchi na vyote vilivyomo ni mali ya BWANA, Dunia na wote wakaao ndani yake.


Wajue ya kuwa Wewe, uitwaye jina lako YEHOVA, Ndiwe peke yako Uliye Juu, juu ya nchi yote.


Nami nitawaleta hata nchi ile ambayo niliinua mkono wangu, niwape Abrahamu, na Isaka, na Yakobo; nitawapa iwe urithi wenu; Mimi ni YEHOVA.


Maana yeye aliye juu, aliyetukuka, akaaye milele; ambaye jina lake ni Mtakatifu; asema hivi; Nakaa mimi mahali palipoinuka, palipo patakatifu; tena pamoja na yeye aliye na roho iliyotubu na kunyenyekea, ili kuzifufua roho za wanyenyekevu, na kuifufua mioyo yao waliotubu.


Nami nikamsikia yule mtu aliyevikwa nguo za kitani, aliyekuwa juu ya maji ya mto, hapo alipoinua mkono wake wa kulia na mkono wake wa kushoto kuelekea mbinguni; akaapa kwa yeye aliye hai milele na milele, ya kwamba itakuwa nyakati tatu na nusu; tena watakapokuwa wamekwisha kuvunja nguvu za hao watu watakatifu, ndipo mambo hayo yote yatakapotimizwa.


Hata mwisho wa siku hizo, mimi, Nebukadneza, nikainua macho yangu kuelekea mbingu, fahamu zangu zikanirudia; nikamhimidi Yeye aliye juu, nikamsifu na kumheshimu Yeye aishiye milele; kwa maana mamlaka yake ni mamlaka ya milele, na ufalme wake hudumu toka kizazi hata kizazi;


Fedha ni mali yangu, na dhahabu ni mali yangu, asema BWANA wa majeshi.


Tazama, mbingu ni mali ya BWANA, Mungu wako, na mbingu za mbingu, na nchi, na vitu vyote vilivyomo.


Maana, nainua mkono wangu mbinguni, Na kusema, Kama Mimi niishivyo milele,


Ikawa alipomuona akayararua mavazi yake, akasema, Ole wangu! Mwanangu, umenitweza sana, nawe u mmoja miongoni mwa hao wanisumbuao; kwa kuwa mimi nimemfunulia BWANA kinywa changu, nami siwezi kurudi nyuma.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo