Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Mwanzo 14:19 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

19 Akambariki, akasema, Abramu na abarikiwe na Mungu Aliye Juu Sana, Muumba mbingu na nchi.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

19 akambariki Abramu akisema, “Abramu na abarikiwe na Mungu Mkuu, Muumba mbingu na dunia!

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

19 akambariki Abramu akisema, “Abramu na abarikiwe na Mungu Mkuu, Muumba mbingu na dunia!

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

19 akambariki Abramu akisema, “Abramu na abarikiwe na Mungu Mkuu, Muumba mbingu na dunia!

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

19 Naye akambariki Abramu, akisema, “Abarikiwe Abramu na Mungu Aliye Juu Sana, Muumba wa mbingu na nchi.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

19 Naye akambariki Abramu, akisema, “Abarikiwe Abramu na Mungu Aliye Juu Sana, Muumba wa mbingu na nchi.

Tazama sura Nakili




Mwanzo 14:19
27 Marejeleo ya Msalaba  

Abramu akamwambia mfalme wa Sodoma, Nimeinua mkono wangu kwa BWANA, Mungu Aliye Juu sana, Muumba mbingu na nchi,


nami nitakuapisha kwa BWANA, Mungu wa mbingu, na Mungu wa nchi, kwamba hutamtwalia mwanangu mke katika binti za Wakanaani ambao nakaa kati yao;


ukaniandalie chakula kitamu namna ile niipendayo, ukaniletee, ili nile; na roho yangu ikubariki, kabla sijafa.


Yakobo akambariki Farao, akatoka mbele ya Farao.


Yusufu akamleta Yakobo babaye ndani akamweka mbele ya Farao, Yakobo akambariki Farao.


Hayo yote ndiyo makabila ya Israeli kumi na mawili. Na hayo ndiyo aliyowaambia baba yao, na kuwabariki; mmoja mmoja kwa baraka zake aliwabariki.


Basi Daudi akatuma wajumbe kwa watu wa Yabesh-gileadi, na kuwaambia, Na mbarikiwe ninyi na BWANA, kwa kuwa mmemtendea bwana wenu fadhili hii, yaani Sauli, mkamzika.


Ee BWANA, ukuu ni wako, na uweza, na utukufu, na ushindi, na enzi; maana vitu vyote vilivyo mbinguni na duniani ni vyako; ufalme ni wako, Ee BWANA, nawe umetukuzwa, u mkuu juu ya vitu vyote.


Hata walipokuja Hezekia na wakuu, na kuyaona yale mafungu, wakamhimidi BWANA, na watu wake Israeli.


Na mbarikiwe ninyi na BWANA, Aliyezifanya mbingu na nchi.


Mbingu ni mbingu za BWANA, Bali nchi amewapa wanadamu.


Nchi na vyote vilivyomo ni mali ya BWANA, Dunia na wote wakaao ndani yake.


Maana kila mnyama-pori ni wangu, Na mifugo juu ya angani elfu.


Nimwendee BWANA na kitu gani, na kuinama mbele za Mungu aliye juu? Je! Nimwendee na sadaka za kuteketezwa, na ndama wa umri wa mwaka mmoja?


Wakati ule Yesu akajibu, akasema, Nakushukuru, Baba, Bwana wa mbingu na nchi, kwa kuwa mambo haya uliwaficha wenye hekima na akili, ukawafunulia watoto wachanga.


Akawakumbatia, akaweka mikono yake juu yao, akawabariki.


Saa ile ile alishangilia katika Roho Mtakatifu, akasema, Nakushukuru, Baba, Bwana wa mbingu na nchi, kwa kuwa mambo haya umewaficha wenye hekima na akili; umewafunulia watoto wachanga; Naam, Baba, kwa kuwa ndivyo ilivyokupendeza.


Akamfuata Paulo na sisi akipiga kelele, akisema, Watu hawa ni watumishi wa Mungu aliye juu, wenye kuwahubiria njia ya wokovu.


Atukuzwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo, aliyetubariki kwa baraka zote za rohoni, katika ulimwengu wa roho, ndani yake Kristo;


Na usifiwe utukufu wa neema yake, ambayo ametuneemesha katika huyo Mpendwa.


Tazama, mbingu ni mali ya BWANA, Mungu wako, na mbingu za mbingu, na nchi, na vitu vyote vilivyomo.


Akamwambia, Mwanangu, ubarikiwe na BWANA; umezidi kuonesha fadhili zako mwisho kuliko mwanzo, kwa vile usivyowafuata vijana, wawe ni maskini au matajiri.


Samweli akamwendea Sauli; naye Sauli akamwambia, Ubarikiwe na BWANA, nimeitimiza amri ya BWANA.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo