Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Mwanzo 14:18 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

18 Na Melkizedeki mfalme wa Salemu akaleta mkate na divai, naye alikuwa kuhani wa Mungu Aliye Juu Sana.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

18 Naye Melkisedeki, mfalme wa mji wa Salemu, ambaye alikuwa kuhani wa Mungu Mkuu, akaleta mkate na divai,

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

18 Naye Melkisedeki, mfalme wa mji wa Salemu, ambaye alikuwa kuhani wa Mungu Mkuu, akaleta mkate na divai,

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

18 Naye Melkisedeki, mfalme wa mji wa Salemu, ambaye alikuwa kuhani wa Mungu Mkuu, akaleta mkate na divai,

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

18 Ndipo Melkizedeki mfalme wa Salemu akaleta mkate na divai. Alikuwa kuhani wa Mungu Aliye Juu Sana.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

18 Ndipo Melkizedeki mfalme wa Salemu alipoleta mkate na divai. Alikuwa kuhani wa Mungu Aliye Juu Sana.

Tazama sura Nakili




Mwanzo 14:18
23 Marejeleo ya Msalaba  

Basi Daudi akatuma wajumbe kwa watu wa Yabesh-gileadi, na kuwaambia, Na mbarikiwe ninyi na BWANA, kwa kuwa mmemtendea bwana wenu fadhili hii, yaani Sauli, mkamzika.


Na divai imfurahishe mtu moyo wake. Aung'aze uso wake kwa mafuta, Na mkate umburudishe mtu moyo wake.


BWANA ameapa, Wala hataghairi, Ndiwe kuhani hata milele, Kwa mfano wa Melkizedeki.


Mtolee Mungu dhabihu za kushukuru; Mtimizie Aliye Juu nadhiri zako.


Nitamwita MUNGU Aliye Juu, Mungu anitimiziaye mambo yangu.


Nitamshukuru BWANA kwa kadiri ya haki yake; Nitaliimbia jina la BWANA aliye juu.


Kibanda chake pia kiko Salemu, Na maskani yake iko Sayuni.


Huko ndiko alikoivunja mishale ya uta, Ngao, upanga, na zana za vita.


Hata neno lile lilipokuwa katika kinywa cha mfalme, sauti ilikuja kutoka mbinguni, ikisema, Ee mfalme Nebukadneza, maneno haya unaambiwa wewe; Ufalme huu umeondoka kwako.


Nimwendee BWANA na kitu gani, na kuinama mbele za Mungu aliye juu? Je! Nimwendee na sadaka za kuteketezwa, na ndama wa umri wa mwaka mmoja?


Hivyo ninyi nanyi mtasongeza sadaka ya kuinuliwa kwa BWANA katika zaka zenu zote, mpokeazo mikononi mwa wana wa Israeli; kwa hiyo mtampa Haruni kuhani hiyo sadaka ya kuinuliwa kwa BWANA.


Asema, yeye asikiaye maneno ya Mungu, Na kuyajua maarifa yake Aliye Juu. Yeye aonaye maono ya Mwenyezi, Akianguka kifudifudi, amefumbuliwa macho,


Akamfuata Paulo na sisi akipiga kelele, akisema, Watu hawa ni watumishi wa Mungu aliye juu, wenye kuwahubiria njia ya wokovu.


Ila Yeye aliye juu hakai katika nyumba zilizojengwa kwa mikono, kama vile asemavyo nabii,


Kwa hiyo kadiri tupatavyo nafasi na tuwatendee watu wote mema; na hasa jamaa ya waaminio.


kisha ametajwa na Mungu kuwa kuhani mkuu kwa mfano wa Melkizedeki.


Kama asemavyo mahali pengine, Ndiwe kuhani milele Kwa mfano wa Melkizedeki.


alimoingia Yesu kwa ajili yetu, mtangulizi wetu, amekuwa kuhani mkuu hata milele kwa mfano wa Melkizedeki.


Kwa maana Melkizedeki huyo, mfalme wa Salemu, kuhani wa Mungu aliye juu, aliyekutana na Abrahamu alipokuwa akirudi katika kuwapiga hao wafalme, akambariki;


Akamwambia, Mwanangu, ubarikiwe na BWANA; umezidi kuonesha fadhili zako mwisho kuliko mwanzo, kwa vile usivyowafuata vijana, wawe ni maskini au matajiri.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo