Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Mika 5:10 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

10 Kisha itakuwa katika siku hiyo, asema BWANA, nitawakatilia mbali farasi wako watoke kati yako, nami nitayaharibu magari yako ya vita;

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

10 Mwenyezi-Mungu asema, “Wakati huo nitawaondoa farasi wenu, na kuyaharibu magari yenu ya farasi.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

10 Mwenyezi-Mungu asema, “Wakati huo nitawaondoa farasi wenu, na kuyaharibu magari yenu ya farasi.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

10 Nitaiharibu miji ya nchi yenu, na kuzibomolea mbali ngome zenu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

10 “Katika siku ile,” asema Mwenyezi Mungu, “nitaangamiza farasi wenu kati yenu, na kubomoa magari yenu ya vita.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

10 “Katika siku ile,” asema bwana, “nitaangamiza farasi zenu katikati yenu na kubomoa magari yenu ya vita.

Tazama sura Nakili




Mika 5:10
9 Marejeleo ya Msalaba  

Tena nchi yao imejaa fedha na dhahabu, wala hapana mwisho wa hazina zao; tena nchi yao imejaa farasi, wala hapana mwisho wa magari yao.


Ni kweli, msaada haufai unaotazamiwa kutoka milimani, makutano yenye mshindo juu ya milima; ni kweli, wokovu wa Israeli ni katika BWANA, Mungu wetu.


Lakini nitairehemu nyumba ya Yuda; nitawaokoa kwa BWANA, Mungu wao; wala sitawaokoa kwa upinde, wala kwa upanga, wala kwa silaha, wala kwa farasi, wala kwa wapanda farasi.


Ashuru hatatuokoa; hatutapanda farasi; wala hatutaiambia tena kazi ya mikono yetu, Ninyi ndinyi miungu yetu; maana kwako wewe wasio na baba hupata rehema.


nami nitakipindua kiti cha enzi cha falme, nami nitaziharibu nguvu za falme za mataifa; nami nitayapindua magari, na hao wapandao ndani yake; farasi na hao wawapandao wataanguka chini; kila mtu kwa upanga wa ndugu yake.


Na gari la vita nitaliondoa liwe mbali na Efraimu, na farasi awe mbali na Yerusalemu, na upinde wa vita utaondolewa mbali; naye atawahubiria mataifa yote habari za amani; na mamlaka yake yatakuwa toka bahari hata bahari, na toka Mto hata miisho ya dunia.


Ila asifanye farasi wake kuwa wengi, wala asiwarudishe watu Misri, ili apate kufanya farasi kuwa wengi; kwa kuwa BWANA amewaambia, Tangu sasa msirudie tena njia ile.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo