Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Mika 1:9 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

9 Kwa maana majeraha yake hayaponyeki; Maana msiba umeijia hata Yuda, Unalifikia lango la watu wangu, Naam, hata Yerusalemu.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

9 Majeraha ya Samaria hayaponyeki, nayo yameipata pia Yuda; yamefikia lango la Yerusalemu, mahali wanapokaa watu wangu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

9 Majeraha ya Samaria hayaponyeki, nayo yameipata pia Yuda; yamefikia lango la Yerusalemu, mahali wanapokaa watu wangu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

9 Majeraha ya Samaria hayaponyeki, nayo yameipata pia Yuda; yamefikia lango la Yerusalemu, mahali wanapokaa watu wangu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

9 Kwa sababu jeraha lake halitibiki; limekuja kwa Yuda. Limefika hasa kwenye lango la watu wangu, hata Yerusalemu kwenyewe.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

9 Kwa sababu jeraha lake halitibiki; limekuja Yuda. Limefika hasa kwenye lango la watu wangu, hata Yerusalemu kwenyewe.

Tazama sura Nakili




Mika 1:9
15 Marejeleo ya Msalaba  

Na malango yake yatalia na kuomboleza, naye atakuwa ukiwa, atakaa chini.


Ikawa, katika mwaka wa kumi na nne wa kutawala kwake mfalme Hezekia, Senakeribu, mfalme wa Ashuru, akapanda ili kupigana na miji yote ya Yuda yenye boma, akaitwaa.


Mfalme wa Ashuru akamtuma amiri toka Lakishi pamoja na jeshi kubwa kwenda hadi Yerusalemu kwa mfalme Hezekia. Naye akasimama karibu na mfereji wa bwawa la juu, lililo katika njia kuu ya kuuendea Uwanda wa Dobi.


Mbona maumivu yangu ni ya daima, na jeraha langu halina dawa, linakataa kuponywa? Je! Yamkini wewe utakuwa kwangu kama kijito kidanganyacho, na kama maji yasiyodumu?


Panda uende Gileadi, ukatwae zeri, Ee binti, bikira wa Misri; unatumia dawa nyingi bure tu; hupati kupona kamwe.


Maana wakazi wa Marothi wanasubiri kwa hamu kupata mema; Lakini maangamizi yameshuka toka kwa BWANA, Yamefika katika lango la Yerusalemu.


Basi, kwa ajili ya hayo, mimi nami nimekupiga kwa pigo liumizalo sana; nimekufanya kuwa ukiwa, kwa sababu ya dhambi zako.


Jeraha lako halipunguziki; donda lako haliponyeki; wote wasikiao habari zako wapiga makofi juu yako; kwa maana ni nani aliyewahi kuukwepa ukatili wako usio na mwisho?


Tufuate:

Matangazo


Matangazo