Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Mhubiri 7:29 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

29 Tazama, hili tu nimeliona; Mungu amemfanya mwanadamu mnyofu, lakini wamepanga mipango mingi.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

29 Tazama, nimegundua jambo hili moja: Kwamba Mungu aliwaumba wanadamu wanyofu, lakini wao wenyewe wamejitafutia matatizo.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

29 Tazama, nimegundua jambo hili moja: Kwamba Mungu aliwaumba wanadamu wanyofu, lakini wao wenyewe wamejitafutia matatizo.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

29 Tazama, nimegundua jambo hili moja: kwamba Mungu aliwaumba wanadamu wanyofu, lakini wao wenyewe wamejitafutia matatizo.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

29 Hili ndilo peke yake nililolipata: Mungu amemuumba mwanadamu mnyofu, lakini mwanadamu amebuni mambo mengi.”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

29 Hili ndilo peke yake nililolipata: Mungu amemuumba mwanadamu mnyofu, lakini mwanadamu amebuni mambo mengi.”

Tazama sura Nakili




Mhubiri 7:29
20 Marejeleo ya Msalaba  

Hiki ndicho kitabu cha vizazi vya Adamu. Siku ile Mungu alipoumba mtu, kwa sura ya Mungu alimfanya;


Wakamkasirisha kwa matendo yao; Tauni ikawashambulia.


Ndivyo walivyotiwa uchafu kwa kazi zao, Wakafanya uasherati kwa matendo yao.


Ee BWANA, Mungu wetu, ndiwe uliyewajibu; Ulikuwa kwao Mungu mwenye kusamehe Ingawa uliwapatiliza matendo yao.


Ni nani aliye kama mwenye hekima; Naye ni nani ajuaye kufasiri neno? Hekima ya mtu humwangaza uso wake, Na ugumu wa uso wake hubadilika.


Kwa maana watu wangu ni wapumbavu, hawanijui; ni watoto waliopungukiwa na akili, wala hawana ufahamu; ni wenye akili katika kutenda mabaya, bali katika kutenda mema hawana maarifa.


Ulikuwa mkamilifu katika njia zako tangu siku ile ulipoumbwa, hata uovu ulipoonekana ndani yako.


Maana hapo zamani sisi nasi tulikuwa hatuna akili, tulikuwa waasi, tumedanganywa, huku tukitumikia tamaa na anasa za namna nyingi, tukiishi katika uovu na husuda, tukichukiza na kuchukiana.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo