Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Methali 31:26 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

26 Hufumbua kinywa chake kwa hekima, Na sheria ya wema iko katika ulimi wake.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

26 Hufungua kinywa kunena kwa hekima, huwashauri wengine kwa wema.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

26 Hufungua kinywa kunena kwa hekima, huwashauri wengine kwa wema.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

26 Hufungua kinywa kunena kwa hekima, huwashauri wengine kwa wema.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

26 Huzungumza kwa hekima, na mafundisho ya kuaminika yapo ulimini mwake.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

26 Huzungumza kwa hekima na mafundisho ya kuaminika yapo ulimini mwake.

Tazama sura Nakili




Methali 31:26
28 Marejeleo ya Msalaba  

Basi wajakazi wake Esta, na wasimamizi wake wa nyumba, wakamjia, wakampasha habari; naye malkia akahuzunika mno; akampelekea Mordekai mavazi, ili kumvika, na kumwondolea gunia lake; lakini yeye hakukubali.


Ikiwa nimepata kibali machoni pa mfalme, na mfalme akiona vema kunipa niombalo, na kunitimizia haja yangu, na aje tena mfalme na Hamani kwenye karamu nitakayowaandalia, nami kesho nitafanya kama vile mfalme alivyosema.


Kinywa cha mwenye haki hutoa hekima; Bali ulimi wa ukaidi utakatiliwa mbali.


Kuna anenaye bila kufikiri, kama kuchoma kwa upanga; Bali ulimi wa mwenye haki ni afya.


Maneno yapendezayo ni kama sega la asali; Ni tamu nafsini, na afya mifupani.


Nyumba na mali ni urithi apatao mtu kwa babaye; Bali mke mwenye busara, mtu hupewa na BWANA.


Kwa uvumilivu mwingi mkuu husadikishwa; Na ulimi laini huvunja mfupa.


Huangalia sana njia za watu wa nyumbani mwake; Wala hali chakula cha uvivu.


Hua wangu, mafichoni mwa jabali, Katika sitara za, magenge Nitazame uso wako, nisikie sauti yako, Maana sauti yako ni tamu na uso wako unapendeza.


Bibi arusi, midomo yako yadondosha asali, Asali na maziwa viko chini ya ulimi wako; Na harufu ya mavazi yako Ni kama harufu ya Lebanoni.


Sheria ya kweli ilikuwa kinywani mwake, wala udhalimu haukuonekana midomoni mwake; alikwenda pamoja nami katika amani na unyofu, na kuwageuza wengi hata wakaacha uovu.


Mariamu akasema, Tazama, mimi ni mjakazi wa Bwana; na iwe kwangu kama ulivyosema. Kisha malaika akaondoka akaenda zake.


Akaanza kunena kwa ujasiri katika sinagogi; hata Priskila na Akila walipomsikia wakampeleka kwao, wakamweleza njia ya Bwana kwa usahihi zaidi.


Watu wote walioketi katika ile baraza wakamkazia macho yao, wakamwona uso wake kuwa kama uso wa malaika.


Neno lolote lililo ovu lisitoke vinywani mwenu, bali lililo jema la kumfaa mwenye kuhitaji, ili liwape neema wanaosikia.


Nendeni kwa hekima mbele yao walio nje, mkiukomboa wakati.


Kadhalika ninyi wake, watiini waume zenu; kusudi, ikiwa wako wasioliamini Neno, wavutwe kwa mwenendo wa wake zao, pasipo lile Neno;


Lakini mkewe akamwambia, Kama BWANA angetaka kutuua hangepokea sadaka ya kuteketezwa, wala sadaka ya unga, mikononi mwetu, wala hangetuonesha mambo hayo yote, wala hangetuambia mambo kama hayo wakati huu.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo