Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Methali 29:18 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

18 Pasipo maono, watu huacha kujizuia; Bali ana heri mtu yule aishikaye sheria.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

18 Pasipo maono ya kinabii watu hukosa nidhamu; heri mtu yule anayeshika sheria.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

18 Pasipo maono ya kinabii watu hukosa nidhamu; heri mtu yule anayeshika sheria.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

18 Pasipo maono ya kinabii watu hukosa nidhamu; heri mtu yule anayeshika sheria.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

18 Mahali pasipo na ufunuo, watu huacha kujizuia, bali ana heri mtu yule anayeitii sheria.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

18 Mahali pasipo na ufunuo, watu kujizuia, bali ana heri mtu yule aishikaye sheria.

Tazama sura Nakili




Methali 29:18
21 Marejeleo ya Msalaba  

Kwa maana BWANA aliinamisha Yuda kwa ajili ya Ahazi mfalme wa Israeli; kwa kuwa yeye aliwafanyia Yuda aibu, na kumwasi BWANA mno.


Heri washikao hukumu, Na kutenda haki sikuzote.


Heri walio kamili njia zao, Waendao katika sheria ya BWANA.


Heri wazitiio shuhuda zake, Wamtafutao kwa moyo wote.


Tena mtumishi wako huonywa kwazo, Katika kuzishika kuna thawabu kuu.


Hatuzioni ishara zetu, wala sasa hakuna nabii, Wala kwetu hakuna ajuaye, hadi lini?


Basi Musa alipoona ya kuwa watu hawa wameasi, maana Haruni amewaacha waasi, na kuwa dhihaka kati ya adui zao,


Yeye aihifadhiye amri huihifadhi nafsi yake; Bali yeye asiyeziangalia njia zake atakufa.


Haitoshi mtumwa kuonywa kwa maneno; Maana ajapoyafahamu hataitika.


Basi, wanangu, nisikilizeni sasa; Maana heri hao wazishikao amri zangu.


Watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa; kwa kuwa wewe umeyakataa maarifa, mimi nami nitakukataa wewe, usiwe kuhani kwangu mimi; kwa kuwa umeisahau sheria ya Mungu wako, mimi nami nitawasahau watoto wako.


Na alipowaona makutano, aliwahurumia, kwa sababu walikuwa wamechoka na kutawanyika kama kondoo wasio na mchungaji.


Lakini yeye alisema, Afadhali, heri walisikiao neno la Mungu na kulishika.


Mkiyajua hayo, heri ninyi mkiyatenda.


Lakini aliyeitazama sheria kamilifu iliyo ya uhuru, na kukaa humo, asiwe msikiaji msahaulifu, bali mtendaji wa kazi, huyo atakuwa heri katika kutenda kwake.


Heri wazifuao nguo zao, ili wawe na haki ya kuuendea huo mti wa uzima, na kuingia mjini kwa milango yake.


Basi, mtoto Samweli akamtumikia BWANA mbele ya Eli. Na neno la BWANA lilikuwa adimu siku zile; hapakuwa na mafunuo dhahiri.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo