Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Methali 29:15 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

15 Fimbo na maonyo hutia hekima; Bali mwana aliyeachiliwa humwaibisha mamaye.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

15 Adhabu na maonyo huleta hekima, lakini mtoto aliyeachwa afanye apendavyo humwaibisha mama yake.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

15 Adhabu na maonyo huleta hekima, lakini mtoto aliyeachwa afanye apendavyo humwaibisha mama yake.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

15 Adhabu na maonyo huleta hekima, lakini mtoto aliyeachwa afanye apendavyo humwaibisha mama yake.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

15 Fimbo ya maonyo hutia hekima, bali mtoto asiyeonywa humwaibisha mama yake.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

15 Fimbo ya maonyo hutia hekima, bali mtoto aliyeachiwa bila maonyo humwaibisha mama yake.

Tazama sura Nakili




Methali 29:15
13 Marejeleo ya Msalaba  

Tena baba yake hakumchukiza wakati wowote kwa kusema, Mbona umefanya hivi? Kisha, alikuwa mtu mzuri sana; naye alizaliwa baada ya Absalomu.


Mwana mwenye hekima humfurahisha babaye; Bali mwana mpumbavu ni mzigo wa mamaye.


Akusanyaye wakati wa joto ni mwana mwenye hekima; Bali asinziaye wakati wa mavuno ni mwana mwenye kuaibisha.


Yeye asiyetumia fimbo yake humchukia mwanawe; Bali yeye ampendaye humrudi mapema.


Azaaye mpumbavu ni kwa huzuni yake mwenyewe; Wala baba wa mpumbavu hana furaha.


Mwana mpumbavu ni huzuni kwa babaye, Na uchungu kwa mamaye aliyemzaa.


Mrudi mwanao, kwa maana liko tumaini; Wala usiikaze nafsi yako kwa kuangamia kwake.


Ujinga umefungwa ndani ya moyo wa mtoto; Lakini fimbo ya adhabu itaufukuzia mbali.


Mlee mtoto katika njia impasayo, Naye hataiacha, hata atakapokuwa mzee.


Mrudi mwanao naye atakustarehesha; Naam, atakufurahisha nafsi yako.


Amwendekezaye mtumwa wake tangu utoto, Mwisho wake atakuwa ni mwanawe.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo