Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Methali 15:33 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

33 Kumcha BWANA ni maonyo ya hekima; Na kabla ya heshima hutangulia unyenyekevu.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

33 Kumcha Mwenyezi-Mungu ni shule ya hekima; kabla ya kuheshimika ni lazima kuwa mnyenyekevu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

33 Kumcha Mwenyezi-Mungu ni shule ya hekima; kabla ya kuheshimika ni lazima kuwa mnyenyekevu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

33 Kumcha Mwenyezi-Mungu ni shule ya hekima; kabla ya kuheshimika ni lazima kuwa mnyenyekevu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

33 Kumcha Mwenyezi Mungu humfundisha mtu hekima, nao unyenyekevu huja kabla ya heshima.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

33 Kumcha bwana humfundisha mtu hekima, nao unyenyekevu huja kabla ya heshima.

Tazama sura Nakili




Methali 15:33
16 Marejeleo ya Msalaba  

Wakati ilipowadia zamu yake Esta, binti Abihaili, mjomba wake Mordekai, ambaye alimtwaa kuwa binti yake, ili aingie kwa mfalme, yeye hakutaka kitu, ila vile vilivyoagizwa na Hegai, msimamizi wake mfalme, aliyewalinda wanawake. Naye huyu Esta alikuwa amepata kibali machoni pa wote waliomwona.


Kisha akamwambia mwanadamu, Tazama, kumcha Bwana ndiyo hekima, Na kujitenga na uovu ndio ufahamu.


Kumcha BWANA ndio mwanzo wa hekima, Wote wafanyao hayo wana ufahamu mzuri, Sifa zake zadumu milele.


Njoni, enyi wana, mnisikilize, Nami nitawafundisha kumcha BWANA.


Kujua hekima na adabu; kutambua maneno ya ufahamu;


Kumcha BWANA ni chanzo cha maarifa, Bali wapumbavu hudharau hekima na adabu.


Akataaye maonyo huidharau nafsi yake mwenyewe; Bali yeye asikilizaye lawama hujipatia ufahamu.


Maandalio ya moyo ni ya mwanadamu; Bali jawabu la ulimi hutoka kwa BWANA.


Kabla ya uharibifu moyo wa mwanadamu hujivuna; Na kabla ya heshima hutangulia unyenyekevu.


Kiburi cha mtu kitamshusha; Bali mwenye roho ya unyenyekevu ataheshimiwa.


Kumcha BWANA ni kuchukia uovu; Kiburi na majivuno, na njia mbovu, Na kinywa cha ukaidi pia nakichukia.


Kwa maana kila ajikwezaye atadhiliwa, naye ajidhiliye atakwezwa.


Jidhilini mbele za Bwana, naye atawakuza.


Vivyo hivyo ninyi vijana, watiini wazee. Naam, ninyi nyote jifungeni unyenyekevu, mpate kuhudumiana; kwa sababu Mungu huwapinga wenye kiburi, lakini huwapa wanyenyekevu neema.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo