Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Methali 1:11 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

11 Wakisema, Haya! Njoo pamoja nasi, Na tuvizie ili kumwaga damu; Tumwotee asiye na hatia, bila sababu;

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

11 Wakisema: “Twende tukamvizie mtu na kumuua; njoo tukawashambulie wasio na hatia!

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

11 Wakisema: “Twende tukamvizie mtu na kumuua; njoo tukawashambulie wasio na hatia!

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

11 Wakisema: “Twende tukamvizie mtu na kumuua; njoo tukawashambulie wasio na hatia!

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

11 Wakisema, “Twende tufuatane; tukamvizie mtu na kumwaga damu, njoo tukavizie nafsi isiyo na hatia;

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

11 Kama wakisema, “Twende tufuatane; tukamvizie mtu na kumwaga damu, njoo tukavizie nafsi isiyo na hatia;

Tazama sura Nakili




Methali 1:11
19 Marejeleo ya Msalaba  

Kama mfano wa simba atakaye kurarua, Kama mwanasimba aoteaye katika maotea yake.


Maana bila sababu wamenifichia wavu, Bila sababu wameichimbia shimo nafsi yangu.


Hukutanika, hujificha, huziangalia nyayo zangu, Kwa kuwa waliniotea ili waniue.


Maana miguu yao huenda mbio maovuni, Nao hufanya haraka ili kumwaga damu.


Na hao hujiotea damu yao wenyewe, Hujinyemelea nafsi zao wenyewe.


Maneno ya waovu huotea damu; Bali kinywa cha wanyofu kitawaokoa.


Ewe mtu mbaya, usiyavizie makao yake mwenye haki; Wala usipaharibu mahali pake pa kupumzika;


Mshiriki wa mwizi huichukia nafsi yake mwenyewe; Asikia maapizo, wala hana neno.


Kuna kizazi cha watu ambao meno yao ni panga; Na vigego vyao ni kama visu. Ili kuwala maskini waondolewe katika nchi, Na wahitaji katika wanadamu.


Lakini mimi nilikuwa kama mwana-kondoo mpole, achukuliwaye kwenda kuchinjwa; wala sikujua ya kuwa wamefanya mashauri kinyume changu, wakisema, Na tuuharibu mti pamoja na matunda yake, na tumkatilie mbali atoke katika nchi ya walio hai, ili jina lake lisikumbukwe tena.


Maana katika watu wangu wameonekana watu waovu; huvizia kama vile watu wategao mitego; hutega mtego, na kunasa watu.


Mtu amchaye Mungu ametoweka, asionekane katika nchi, wala hapana mtu mwenye adili katika wanadamu; wote huotea ili kumwaga damu; kila mtu humwinda ndugu yake kwa wavu.


Lakini litimie lile neno lililoandikwa katika torati yao, Walinichukia bure.


Basi sasa ninyi pamoja na wazee wa baraza mwambieni jemadari amlete chini kwenu, kana kwamba mnataka kujua habari zake vizuri zaidi; na sisi tuko tayari kumwua kabla hajakaribia.


na kumwomba fadhili juu yake, kwamba atoe amri aletwe Yerusalemu, wapate kumwotea na kumwua njiani.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo