Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Matendo 7:9 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

9 Wale wazee wetu wakimwonea wivu Yusufu, wakamwuza aende Misri. Mungu akawa pamoja naye,

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

9 “Wale mababu walimwonea wivu Yosefu, wakamwuza utumwani Misri. Lakini Mungu alikuwa pamoja naye,

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

9 “Wale mababu walimwonea wivu Yosefu, wakamwuza utumwani Misri. Lakini Mungu alikuwa pamoja naye,

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

9 “Wale mababu walimwonea wivu Yosefu, wakamwuza utumwani Misri. Lakini Mungu alikuwa pamoja naye,

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

9 “Kwa sababu hao baba zetu wa zamani walimwonea wivu Yusufu ndugu yao, walimuuza kama mtumwa huko Misri. Lakini Mungu alikuwa pamoja naye.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

9 “Kwa sababu wazee wetu walimwonea wivu Yusufu ndugu yao, walimuuza kama mtumwa huko Misri. Lakini Mungu alikuwa pamoja naye.

Tazama sura Nakili




Matendo 7:9
14 Marejeleo ya Msalaba  

BWANA akawa pamoja na Yusufu, naye akasitawi; naye alikuwa katika nyumba ya bwana wake, yule Mmisri.


Ikawa tokea wakati alipomweka kuwa msimamizi wa nyumba yake, na vyote vilivyomo, BWANA akabariki nyumba ya yule Mmisri kwa ajili ya Yusufu. Baraka za BWANA zikawa juu ya vyote alivyokuwa navyo katika nyumba, na katika shamba.


Yusufu akawaambia ndugu zake, Karibuni kwangu; basi, wakakaribia. Akasema, Mimi ni Yusufu, ndugu yenu, ambaye mliniuza kwenda Misri.


Alimpeleka mtu mbele yao, Yusufu aliuzwa utumwani.


usiogope, kwa maana mimi ni pamoja nawe; usifadhaike, kwa maana mimi ni Mungu wako; nitakutia nguvu, naam, nitakusaidia, naam, nitakushika kwa mkono wa kulia wa haki yangu.


Upitapo katika maji mengi nitakuwa pamoja nawe; na katika mito, haitakugharikisha; uendapo katika moto, hutateketea; wala mwali wa moto hautakuunguza.


Lakini sasa uwe jasiri, Ee Zerubabeli, asema BWANA; nawe uwe jasiri, Ee Yoshua, mwana wa Yehosadaki, kuhani mkuu, nanyi iweni jasiri, enyi watu wote wa nchi hii, asema BWANA; mkafanye kazi, kwa kuwa mimi ni pamoja nanyi, asema BWANA wa majeshi;


Kwa maana alijua ya kuwa wamemtoa kwa ajili ya husuda.


Upendo huvumilia, hufadhili; upendo hauhusudu; upendo hautakabari; haujivuni;


Tufuate:

Matangazo


Matangazo