Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Matendo 7:60 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

60 Akapiga magoti, akalia kwa sauti kuu, Bwana, usiwahesabie dhambi hii. Akiisha kusema haya akalala. Na Sauli alikuwa akiona kitendo cha kuuawa kwake kuwa sawa.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

60 Akapiga magoti, akalia kwa sauti kubwa: “Bwana, usiwalaumu kwa sababu ya dhambi hii.” Baada ya kusema hivyo, akafa.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

60 Akapiga magoti, akalia kwa sauti kubwa: “Bwana, usiwalaumu kwa sababu ya dhambi hii.” Baada ya kusema hivyo, akafa.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

60 Akapiga magoti, akalia kwa sauti kubwa: “Bwana, usiwalaumu kwa sababu ya dhambi hii.” Baada ya kusema hivyo, akafa.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

60 Kisha akapiga magoti, akalia kwa sauti kubwa akasema, “Bwana, usiwahesabie dhambi hii.” Baada ya kusema hayo, akalala.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

60 Kisha akapiga magoti, akalia kwa sauti kubwa, akasema, “Bwana Isa, usiwahesabie dhambi hii.” Baada ya kusema hayo, akalala.

Tazama sura Nakili




Matendo 7:60
23 Marejeleo ya Msalaba  

Na wakati wa sadaka ya jioni nikainuka baada ya kunyenyekea kwangu, nguo yangu na joho langu zimeraruliwa, nikaanguka magotini nikakunjua mikono yangu mbele za BWANA, Mungu wangu;


Tena, wengi wa hao wanaolala katika mavumbi ya nchi wataamka, wengine wapate uzima wa milele, wengine aibu na kudharauliwa milele.


Hata Danieli, alipojua ya kuwa yale maandiko yamekwisha kutiwa sahihi, akaingia nyumbani mwake, (na madirisha katika chumba chake yalikuwa yamefunguliwa kuelekea Yerusalemu;) akapiga magoti mara tatu kila siku, akasali, akashukuru mbele za Mungu wake, kama alivyokuwa akifanya tokea hapo.


makaburi yakafunuka; ikainuka miili mingi ya watakatifu waliolala;


lakini mimi nawaambia, Wapendeni adui zenu, waombeeni wanaowaudhi,


Mwenyewe akajitenga nao kama kiasi cha kutupa jiwe, akapiga magoti akaomba,


Yesu akasema, Baba, uwasamehe, kwa kuwa hawajui watendalo. Wakagawa mavazi yake, wakipiga kura.


wabarikieni wale ambao wawalaani ninyi, waombeeni wale ambao wawaonea ninyi.


Aliyasema hayo; kisha, baada ya hayo, akawaambia, Rafiki yetu, Lazaro, amelala; lakini ninakwenda nipate kumwamsha.


Kwa maana Daudi, akiisha kulitumikia shauri la Mungu katika kizazi chake, alilala, akawekwa pamoja na baba zake, akaona uharibifu.


Alipokwisha kunena haya akapiga magoti, akaomba pamoja nao wote.


Hata tulipotimiza siku zile tukaondoka tukaenda zetu, na watu wote, pamoja na wake zao na watoto wao, wakatusindikiza mpake nje ya mji, tukapiga magoti pwani tukaomba;


Petro akawatoa nje wote, akapiga magoti, akaomba, kisha akaelekea yule maiti, akanena, Tabitha, inuka. Naye akafumbua macho yake, na alipomwona Petro akajiinua, akaketi.


Kwa sababu hiyo wako wengi kwenu walio wagonjwa na dhaifu, na watu kadhaa wamelala.


Na hapo wao nao waliolala katika Kristo wamepotea.


Lakini sasa Kristo amefufuka katika wafu, limbuko lao waliolala.


Angalieni, nawaambia ninyi siri; hatutalala sote, lakini sote tutabadilika,


baadaye aliwatokea ndugu zaidi ya mia tano pamoja; katika hao wengi wanaishi hata sasa, ila baadhi yao wamelala;


ambaye alikufa kwa ajili yetu, ili tuishi pamoja naye, iwe tunakesha au tunalala.


Katika utetezi wangu wa kwanza hakuna mtu aliyesimama upande wangu, bali wote waliniacha; naomba wasihesabiwe hatia kwa jambo hilo.


na kusema, Iko wapi ahadi ile ya kuja kwake? Kwa maana, tangu hapo babu zetu walipolala, vitu vyote vinakaa hali iyo hiyo, tangu mwanzo wa kuumbwa.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo