Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Matendo 25:19 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

19 bali walikuwa na maswali tofauti tofauti juu yake katika dini yao wenyewe, na kuhusu mtu mmoja Yesu, aliyekuwa amekwisha kufa, ambaye Paulo alikazania kusema kuwa yuko hai.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

19 Ila tu walikuwa na mabishano kadhaa pamoja naye kuhusu dini yao na kuhusu mtu mmoja aitwaye Yesu ambaye alikufa, lakini Paulo anashikilia kwamba yu hai.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

19 Ila tu walikuwa na mabishano kadhaa pamoja naye kuhusu dini yao na kuhusu mtu mmoja aitwaye Yesu ambaye alikufa, lakini Paulo anashikilia kwamba yu hai.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

19 Ila tu walikuwa na mabishano kadhaa pamoja naye kuhusu dini yao na kuhusu mtu mmoja aitwaye Yesu ambaye alikufa, lakini Paulo anashikilia kwamba yu hai.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

19 Badala yake walikuwa na vipengele fulani vya kutokukubaliana naye kuhusu dini yao na kuhusu mtu aitwaye Isa aliyekufa, lakini Paulo alidai kwamba yu hai.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

19 Badala yake walikuwa na vipengele fulani vya kutokukubaliana naye kuhusu dini yao na juu ya mtu mmoja aitwaye Isa, ambaye alikufa, lakini yeye Paulo alidai kwamba yu hai.

Tazama sura Nakili




Matendo 25:19
14 Marejeleo ya Msalaba  

kuanza tangu ubatizo wa Yohana, hata siku ile alipochukuliwa kwetu kwenda juu, inapasa mmoja wao awe shahidi wa kufufuka kwake pamoja nasi.


Kwa maana ameweka siku atakayowahukumu walimwengu kwa haki, kwa mtu yule aliyemchagua; naye amewapa watu wote uthabiti wa mambo haya kwa kumfufua katika wafu.


bali ikiwa ni hoja juu ya maneno na majina na sheria yenu, liangalieni ninyi wenyewe, maana mimi sitaki kuwa mwamuzi wa mambo hayo.


Wakafika Efeso, akawaacha huko. Yeye mwenyewe akaingia katika sinagogi, akahojiana na Wayahudi.


Yesu huyo Mungu alimfufua, na sisi sote tu mashahidi wake.


nikaona kwamba ameshitakiwa kwa ajili ya maswali ya sheria yao, wala hakushitakiwa neno lolote la kustahili kuuawa wala kufungwa.


Na wale waliomshitaki waliposimama hawakuleta neno lolote baya, kama nilivyodhani,


Alipokuja, wale Wayahudi walioshuka kutoka Yerusalemu wakasimama karibu naye wakaleta mashitaka mengi mazito juu yake, wasiyoweza kuyayakinisha.


Hasa kwa sababu wewe unajua sana desturi na maswali yote waliyo nayo Wayahudi; kwa sababu hiyo nakuomba unisikilize kwa uvumilivu.


na aliye hai; nami nilikuwa nimekufa, na tazama, ni hai hata milele na milele. Nami ninazo funguo za mauti, na za kuzimu.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo