Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Matendo 14:11 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

11 Na makutano walipoona aliyoyafanya Paulo wakapaza sauti zao, wakisema kwa lugha ya Kilikaonia, Miungu wametushukia kwa mifano ya wanadamu.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

11 Umati wa watu walipoona alichofanya Paulo, walianza kupiga kelele kwa lugha ya Kilukaonia: “Miungu imetujia katika sura za binadamu!”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

11 Umati wa watu walipoona alichofanya Paulo, walianza kupiga kelele kwa lugha ya Kilukaonia: “Miungu imetujia katika sura za binadamu!”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

11 Umati wa watu walipoona alichofanya Paulo, walianza kupiga kelele kwa lugha ya Kilukaonia: “Miungu imetujia katika sura za binadamu!”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

11 Umati ule wa watu walipoona yaliyokuwa yamefanywa na Paulo, wakapaza sauti, wakasema kwa lugha yao ya Kilikaonia, “Miungu imetushukia katika umbo la binadamu!”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

11 Ule umati wa watu ulipoona yaliyokuwa yamefanywa na Paulo, wakapiga kelele kwa lugha yao ya Kilikaonia wakasema, “Miungu imetushukia katika umbo la binadamu!”

Tazama sura Nakili




Matendo 14:11
6 Marejeleo ya Msalaba  

Maana wewe hukutumwa kwa watu wa lugha isiyoeleweka, ama wa lugha ngumu, bali kwa nyumba ya Israeli;


Watu wakapiga kelele, wakisema, Ni sauti ya mungu, si sauti ya mwanadamu.


Wakamwita Barnaba, Zeu, na Paulo, Herme, kwa sababu ndiye aliyekuwa mnenaji.


wao wakapata habari wakakimbilia Listra na Derbe, miji ya Likaonia, na nchi zilizo kandokando;


Wao wakadhani ya kuwa atavimba au kuanguka chini kwa kufa ghafla; na wakiisha kumwangalia sana, na kuona kwamba halimpati dhara lolote, wakageuka, wakasema kwamba yeye ni mungu.


Wote wakamsikiliza tangu mdogo hata mkubwa, wakisema, Mtu huyu ni uweza wa Mungu, aliye Mkuu.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo