Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Matendo 11:17 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

17 Basi ikiwa Mwenyezi Mungu amewapa wao karama ile ile aliyotupa sisi tuliomwamini Bwana Yesu Kristo, mimi ni nani niweze kumpinga Mungu?

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

17 Basi, kama Mungu amewapa pia watu wa mataifa mengine kipawa kilekile alichotupa sisi tulipomwamini Bwana Yesu Kristo, je, mimi ni nani hata nijaribu kumpinga Mungu?”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

17 Basi, kama Mungu amewapa pia watu wa mataifa mengine kipawa kilekile alichotupa sisi tulipomwamini Bwana Yesu Kristo, je, mimi ni nani hata nijaribu kumpinga Mungu?”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

17 Basi, kama Mungu amewapa pia watu wa mataifa mengine kipawa kilekile alichotupa sisi tulipomwamini Bwana Yesu Kristo, je, mimi ni nani hata nijaribu kumpinga Mungu?”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

17 Basi ikiwa Mungu aliwapa hawa watu kipawa kile kile alichotupatia sisi tuliomwamini Bwana Isa Al-Masihi, mimi ni nani hata nifikirie kuwa ningeweza kumpinga Mungu?”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

17 Basi ikiwa Mungu aliwapa hawa watu kipawa kile kile alichotupa sisi tuliomwamini Bwana Isa Al-Masihi, mimi ni nani hata nifikirie kuwa ningeweza kumpinga Mwenyezi Mungu?”

Tazama sura Nakili




Matendo 11:17
14 Marejeleo ya Msalaba  

Kwa nini unapingana naye, ukisema, Hatajibu hata neno langu moja?


Je! Mwenye hoja atashindana na Mwenyezi? Mwenye kujadiliana na Mungu, na ajibu yeye.


na watu wote wanaokaa duniani wamehesabiwa kuwa si kitu, naye hufanya kama atakavyo, katika jeshi la mbinguni, na katika hao wanaokaa duniani; wala hapana awezaye kuuzuia mkono wake, wala kumwuliza, Unafanya nini wewe?


Na wale waliotahiriwa, walioamini, wakashangaa, watu wote waliokuja pamoja na Petro, kwa sababu Mataifa nao wamemwagiwa kipawa cha Roho Mtakatifu.


Ni nani awezaye kuzuia maji, hawa wasibatizwe, watu waliopokea Roho Mtakatifu vile vile kama sisi?


Ikawa nilipoanza kunena, Roho Mtakatifu akawashukia kama alivyotushukia sisi mwanzo.


lakini ikiwa imetoka kwa Mungu hamwezi kuivunja; msije mkaonekana kuwa mnapigana na Mungu.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo