Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Kutoka 8:22 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

22 Nami siku hiyo nitatenga nchi ya Gosheni, watu wangu wanayokaa, ili hao inzi wasiwe huko; ili kwamba upate kujua wewe ya kuwa mimi ndimi BWANA kati ya dunia.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

22 Lakini siku hiyo sehemu ya Gosheni wanakoishi watu wangu nitaikinga: Humo nzi hao hawatakuwamo. Hapo ndipo utakapotambua kwamba mimi Mwenyezi-Mungu natenda mambo nchini mwako.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

22 Lakini siku hiyo sehemu ya Gosheni wanakoishi watu wangu nitaikinga: Humo nzi hao hawatakuwamo. Hapo ndipo utakapotambua kwamba mimi Mwenyezi-Mungu natenda mambo nchini mwako.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

22 Lakini siku hiyo sehemu ya Gosheni wanakoishi watu wangu nitaikinga: humo nzi hao hawatakuwamo. Hapo ndipo utakapotambua kwamba mimi Mwenyezi-Mungu natenda mambo nchini mwako.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

22 “ ‘Lakini siku ile nitafanya kitu tofauti katika nchi ya Gosheni, ambapo watu wangu wanaishi, hapatakuwa na makundi ya inzi, ili mpate kujua kwamba Mimi, Mwenyezi Mungu, niko katika nchi hii.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

22 “ ‘Lakini siku ile nitafanya kitu tofauti katika nchi ya Gosheni, ambapo watu wangu wanaishi, hapatakuwepo na makundi ya mainzi, ili mpate kujua kwamba Mimi, bwana, niko katika nchi hii.

Tazama sura Nakili




Kutoka 8:22
19 Marejeleo ya Msalaba  

Semeni, Watumishi wako tumekuwa wachunga wanyama tangu ujana wetu, na hata leo, sisi, na baba zetu; mpate kukaa katika nchi ya Gosheni; maana kila mchunga wanyama ni chukizo kwa Wamisri.


BWANA atainyosha toka Sayuni Fimbo ya nguvu zako. Uwe na enzi kati ya adui zako;


Lakini Mungu ni mfalme wangu tokea zamani, Afanyaye mambo ya wokovu katikati ya nchi.


hawakupata kuonana mtu na mwenziwe, wala hakuondoka mtu mahali alipokuwa muda wa siku tatu; lakini wana wa Israeli wote walikuwa na mwanga makaoni mwao.


Na ile damu itakuwa ishara kwenu katika zile nyumba mtakazokuwamo; nami nitakapoiona ile damu, nitapita juu yenu, lisiwapate pigo lolote likawaharibu, nitakapoipiga nchi ya Misri.


Sasa basi ikiwa mtaitii sauti yangu kweli kweli, na kulishika agano langu, hapo ndipo mtakapokuwa tunu kwangu kuliko makabila yote ya watu; maana dunia yote pia ni mali yangu,


Maana, kwa siku sita BWANA alifanya mbingu, na nchi, na bahari, na vyote vilivyomo, akastarehe siku ya saba; kwa hiyo BWANA akaibarikia siku ya Sabato akaitakasa.


BWANA asema, Katika jambo hili utanijua ya kuwa mimi ndimi BWANA; tazama, nitayapiga haya maji yaliyo mtoni kwa fimbo hii niliyo nayo mkononi mwangu, nayo yatageuzwa kuwa damu.


Na Wamisri watajua ya kuwa mimi ndimi BWANA, hapo nitakapounyosha mkono wangu juu ya Misri na kuwatoa wana wa Israeli watoke kati yao.


Akamwambia, Kesho, Akasema, Na yawe kama neno lako; ili upate kujua ya kwamba hapana mwingine mfano wa BWANA, Mungu wetu.


Au kwamba huwapi ruhusa watu wangu, tazama, nitaleta inzi wengi sana juu yako wewe, na juu ya watumishi wako, na juu ya watu wako, nao wataingia ndani ya nyumba zako; na nyumba za Wamisri zitajawa na inzi wengi sana, na nchi nayo ambayo wa juu yake.


Nami nitatia mpaka kati ya watu wangu na watu wako; ishara hiyo italetwa kesho.


Katika nchi ya Gosheni peke yake, walikokaa wana wa Israeli, haikuwako mvua ya mawe.


Musa akamwambia, Mara nitakapotoka mjini nitamwinulia BWANA mikono yangu; na hizo ngurumo zitakoma, wala haitanyesha mvua ya mawe tena; ili upate kujua ya kuwa dunia hii ni ya BWANA.


Kisha BWANA atawatenga wanyama wa Israeli na wanyama wa Misri; wala hakitakufa kitu chochote cha wana wa Israeli.


BWANA akalifanya jambo hilo siku ya pili, na wanyama wote wa kufugwa wa Misri wakafa; lakini katika wanyama wa wana wa Israeli hakufa hata mmoja.


Hivyo ndivyo nitakavyotekeleza hukumu katika Misri; nao watajua ya kuwa mimi ndimi BWANA.


Ndipo mtakaporudi, nanyi mtapambanua kati ya wenye haki na waovu, kati ya yeye amtumikiaye Mungu na yeye asiyemtumikia.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo