Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Kutoka 5:13 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

13 Wasimamizi wao wakawahimiza, wakisema, Timizeni kazi zenu, shughuli zenu za kila siku, kama wakati ule majani yalipokuwapo.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

13 Nao Wanyapara wakakazana wakisema, “Timizeni kazi yenu ya kila siku kama hapo awali mlipoletewa nyasi.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

13 Nao Wanyapara wakakazana wakisema, “Timizeni kazi yenu ya kila siku kama hapo awali mlipoletewa nyasi.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

13 Nao Wanyapara wakakazana wakisema, “Timizeni kazi yenu ya kila siku kama hapo awali mlipoletewa nyasi.”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

13 Viongozi wa watumwa wakasisitiza wakisema, “Timizeni kazi mnayotakiwa kwa kila siku, kama wakati ule mlipokuwa mkipewa nyasi.”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

13 Viongozi wa watumwa wakasisitiza, wakisema, “Timizeni kazi mnayotakiwa kwa kila siku, kama wakati ule mlipokuwa mkipewa nyasi.”

Tazama sura Nakili




Kutoka 5:13
7 Marejeleo ya Msalaba  

Wakaishika sikukuu ya vibanda, kama ilivyoandikwa, wakatoa sadaka za kuteketezwa za kila siku kwa hesabu yake, kama ilivyoagizwa, kama ilivyopasa kila siku;


Yeye hudharau mshindo wa mji, Wala hasikii kelele zake msimamizi.


Basi wakaweka wasimamizi juu yao wawatese kwa mizigo yao. Nao wakamjengea Farao miji ya kuwekea akiba, Pithomu na Ramesesi.


Nendeni wenyewe, jipatieni majani hapo mtakapoyaona; kwa maana kazi yenu haitapunguzwa hata kidogo.


Basi hao watu wakatawanyika katika nchi yote ya Misri ili wapate kukusanya takataka ya mashamba badala ya majani.


Na wanyapara wa wana wa Israeli, ambao wasimamizi wa Farao wamewaweka juu yao, wakapigwa, wakiambiwa, Kwa nini hamkutimiza kazi yenu jana na leo; kwa kufanya matofali kama hapo kwanza?


Na siku ile ile Farao akawaamuru wasimamizi wa watu, na wanyapara wao, akisema,


Tufuate:

Matangazo


Matangazo