Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Kutoka 40:9 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

9 Kisha utayatwaa mafuta ya kutiwa, na kuitia mafuta hiyo maskani, na kila kitu kilicho ndani yake, na kuiweka iwe takatifu, na vyombo vyake vyote; nayo itakuwa takatifu.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

9 “Kisha, utaliweka wakfu hema takatifu pamoja na vyombo vyake vyote kwa kuvipaka yale mafuta ya kupaka, nalo litakuwa takatifu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

9 “Kisha, utaliweka wakfu hema takatifu pamoja na vyombo vyake vyote kwa kuvipaka yale mafuta ya kupaka, nalo litakuwa takatifu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

9 “Kisha, utaliweka wakfu hema takatifu pamoja na vyombo vyake vyote kwa kuvipaka yale mafuta ya kupaka, nalo litakuwa takatifu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

9 “Chukua mafuta ya upako, upake maskani ya Mungu pamoja na kila kitu kilicho ndani yake; iweke wakfu pamoja na vitu vyote vilivyomo, nayo itakuwa takatifu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

9 “Chukua mafuta ya upako, ipake Maskani ya Mungu pamoja na kila kitu kilichomo ndani yake; iweke wakfu pamoja na vitu vyote vilivyomo ndani mwake, nayo itakuwa takatifu.

Tazama sura Nakili




Kutoka 40:9
16 Marejeleo ya Msalaba  

Umeipenda haki; Umeichukia dhuluma. Kwa hiyo MUNGU, Mungu wako, amekutia mafuta, Mafuta ya furaha kuliko wenzako.


Kisha akayafanya hayo mafuta matakatifu ya kutiwa, na ule uvumba safi wa viungo vya manukato vizuri, kwa kuandama kazi ya mtengezaji manukato.


na madhabahu ya shaba, na wavu wake wa shaba, na miti yake, na vyombo vyake vyote, na birika na kitako chake;


Kisha utausimamisha ukuta wa ua kuuzunguka pande zote, na kuitundika sitara ya lango la ua.


Na Roho ya BWANA itakaa juu yake, roho ya hekima na ufahamu, roho ya shauri na uweza, roho ya maarifa na ya kumcha BWANA;


Roho ya Bwana MUNGU i juu yangu; kwa sababu BWANA amenitia mafuta niwahubirie wanyenyekevu habari njema; amenituma ili kuwatibu waliovunjika moyo, kuwatangazia mateka uhuru wao, na hao waliofungwa habari za kufunguliwa kwao.


Wewe ulikuwa kerubi mwenye kutiwa mafuta afunikaye; nami nilikuweka hata ukawa juu ya mlima mtakatifu wa Mungu, umetembea huku na huko kati ya mawe ya moto.


Kisha Musa akatwaa hayo mafuta matakatifu ya kutia, akatia mafuta maskani, na vyote vilivyokuwamo, na kuvitakasa.


Ilikuwa siku hiyo Musa alipokwisha kuisimamisha maskani, na kuitia mafuta, na kuitakasa, na vyombo vyake vyote, na hiyo madhabahu na vyombo vyake vyote, na kuvitia mafuta, na kuvitakasa;


Naye Yesu alipokwisha kubatizwa mara aliibuka kutoka majini na tazama, mbingu zikamfunukia, akamwona Roho wa Mungu akishuka kama hua, na kutua juu yake;


Kwa kuwa yeye aliyetumwa na Mungu huyanena maneno ya Mungu; kwa sababu hamtoi Roho kwa kipimo.


naye ndiye aliyetutia mhuri akatupa arabuni ya Roho mioyoni mwetu.


atufarijiye katika dhiki zetu zote ili nasi tupate kuwafariji wale walio katika dhiki za namna zote, kwa faraja hizo, tunazofarijiwa na Mungu.


Na ile hema nayo na vyombo vyote vya ibada alivinyunyizia damu vivyo hivyo.


Nanyi mmepakwa mafuta na Yeye aliye Mtakatifu nanyi mnajua nyote.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo