Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Kutoka 40:38 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

38 Kwa maana lile wingu la BWANA lilikuwa juu ya maskani wakati wa mchana, na mlikuwa na moto ndani yake wakati wa usiku, mbele ya macho ya nyumba ya Israeli katika safari zao zote.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

38 Katika safari zao zote, Waisraeli waliweza kuliona lile wingu la Mwenyezi-Mungu juu ya hema wakati wa mchana na ule moto ukiwaka juu yake usiku.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

38 Katika safari zao zote, Waisraeli waliweza kuliona lile wingu la Mwenyezi-Mungu juu ya hema wakati wa mchana na ule moto ukiwaka juu yake usiku.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

38 Katika safari zao zote, Waisraeli waliweza kuliona lile wingu la Mwenyezi-Mungu juu ya hema wakati wa mchana na ule moto ukiwaka juu yake usiku.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

38 Kwa hiyo wingu la Mwenyezi Mungu lilikuwa juu ya maskani ya Mungu mchana, na moto ulikuwa katika hilo wingu wakati wa usiku, machoni pa nyumba yote ya Israeli siku zote za safari zao.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

38 Kwa hiyo wingu la bwana lilikuwa juu ya maskani mchana, na moto ulikuwa katika hilo wingu wakati wa usiku, machoni pa nyumba yote ya Israeli siku zote za safari zao.

Tazama sura Nakili




Kutoka 40:38
10 Marejeleo ya Msalaba  

Kwa maana mimi sikukaa ndani ya nyumba, tangu siku ile niliyowatoa wana wa Israeli katika Misri, hata leo, lakini nimekaa katika hema na maskani.


Alitandaza wingu liwe kifuniko, Na moto ili uwaangazie usiku.


Akawaongoza kwa wingu mchana, Na usiku kucha kwa nuru ya moto.


BWANA naye akawatangulia mchana ndani ya wingu mfano wa nguzo, ili awaongoze njia; na usiku, ndani ya moto mfano wa nguzo, ili kuwapa nuru; wapate kusafiri mchana na usiku;


ile nguzo ya wingu haikuondoka mchana, wala ile nguzo ya moto haikuondoka usiku, mbele ya hao watu.


Na wingu la BWANA lilikuwa juu yao mchana hapo waliposafiri kwenda mbele kutoka kambini.


wasisaze kitu chake chochote hadi asubuhi, wala wasimvunje mfupa wake; kama hiyo sheria yote ya Pasaka ilivyo ndivyo watakavyoishika.


Na siku hiyo maskani iliposimamishwa, lile wingu likaifunika maskani, yaani, hema ya kukutania; wakati wa jioni likawa juu ya maskani, mfano wa moto, hata asubuhi.


Ndivyo ilivyokuwa sikuzote; lile wingu liliifunika kwa mfano wa moto usiku.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo