Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Kutoka 40:18 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

18 Musa akaisimamisha maskani, akaviweka vitako vyake, akazisimamisha mbao zake akayatia mataruma yake, akazisimamisha nguzo zake.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

18 Mose aliweka vikalio vyake, akainua mbao zake, akashikamanisha pau zake na kusimamisha nguzo zake.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

18 Mose aliweka vikalio vyake, akainua mbao zake, akashikamanisha pau zake na kusimamisha nguzo zake.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

18 Mose aliweka vikalio vyake, akainua mbao zake, akashikamanisha pau zake na kusimamisha nguzo zake.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

18 Musa alipoweka wakfu maskani ya Mungu, aliweka vitako mahali pake, akasimamisha mihimili, akatia mataruma na kusimamisha nguzo.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

18 Musa alipoweka wakfu Maskani ya Mungu, aliweka vitako mahali pake, akasimamisha mihimili, akatia mataruma na kusimamisha nguzo.

Tazama sura Nakili




Kutoka 40:18
15 Marejeleo ya Msalaba  

Kwa maana mimi sikukaa ndani ya nyumba, tangu siku ile niliyowatoa wana wa Israeli katika Misri, hata leo, lakini nimekaa katika hema na maskani.


Hata mwezi wa kwanza wa mwaka wa pili, siku ya kwanza ya mwezi maskani ile ilisimamishwa.


Akaitanda hema juu ya maskani, akakitia kifuniko cha hema juu yake; kama BWANA alivyomwamuru Musa.


Siku ya kwanza ya mwezi wa kwanza utaisimamisha hiyo maskani ya hema ya kukutania.


Wala hapana mwenyeji atakayesema, Mimi mgonjwa; watu wakaao humo watasamehewa uovu wao.


Nami nitaiweka maskani yangu kati yenu; wala roho yangu haitawachukia.


Nami nakuambia, Wewe ndiwe Petro, na juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu; wala milango ya kuzimu haitalishinda.


Naye Neno alifanyika mwili, akakaa kwetu; nasi tukauona utukufu wake, utukufu kama wa Mwana pekee atokaye kwa Baba; amejaa neema na kweli.


Lakini ulipowadia utimilifu wa wakati, Mungu alimtuma Mwanawe ambaye amezaliwa na mwanamke, amezaliwa chini ya sheria,


Lakini nikikawia, upate kujua jinsi iwapasavyo watu kuenenda katika nyumba ya Mungu, iliyo kanisa la Mungu aliye hai, nguzo na msingi wa kweli.


Nanyi mnalindwa na nguvu za Mungu kwa njia ya imani ili mpate wokovu ulio tayari kufunuliwa wakati wa mwisho.


Nikasikia sauti kubwa kutoka katika kile kiti cha enzi ikisema, Tazama, maskani ya Mungu ni pamoja na wanadamu, naye atafanya maskani yake pamoja nao, nao watakuwa watu wake. Naye Mungu mwenyewe atakuwa pamoja nao.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo