Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Kutoka 4:24 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

24 Ndipo walipokuwa njiani mahali pa kulala, BWANA akakutana naye, akataka kumwua.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

24 Akiwa bado njiani kurudi Misri, Mose alikuwa mahali pa kulala wageni; basi, Mungu alikutana naye na kutaka kumuua.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

24 Akiwa bado njiani kurudi Misri, Mose alikuwa mahali pa kulala wageni; basi, Mungu alikutana naye na kutaka kumuua.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

24 Akiwa bado njiani kurudi Misri, Mose alikuwa mahali pa kulala wageni; basi, Mungu alikutana naye na kutaka kumuua.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

24 Musa alipokuwa mahali pa kulala wageni akiwa njiani kurudi Misri, Mwenyezi Mungu akakutana naye, akataka kumuua.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

24 Musa alipokuwa mahali pa kulala wageni akiwa njiani kurudi Misri, bwana akakutana naye, akataka kumuua.

Tazama sura Nakili




Kutoka 4:24
8 Marejeleo ya Msalaba  

Na mwanamume mwenye govi asiyetahiriwa nyama ya govi lake, mtu yule atatengwa na watu wake; amelivunja agano langu.


Mmoja wao alipofungua gunia lake ili ampe punda wake chakula katika nyumba ya wageni, aliiona fedha yake; kumbe! Iko kinywani mwa gunia lake.


Na alipokuwa amekwenda zake, simba alimkuta njiani, akamwua. Maiti yake ikatupwa njiani, na yule punda akasimama karibu naye; na yule simba naye akasimama karibu na maiti.


Daudi akainua macho yake, akamwona huyo malaika wa BWANA amesimama kati ya nchi na mbingu, naye alikuwa na upanga wazi mkononi, umenyoshwa juu ya Yerusalemu. Ndipo Daudi na wazee wakaanguka kifudifudi, nao wamevaa nguo za magunia.


Nao watakusikia sauti yako; nawe utakwenda, wewe na wazee wa Israeli kwa mfalme wa Misri, na kumwambia, BWANA Mungu wa Waebrania, amekutana nasi; basi sasa twakuomba, tupe ruhusa twende mwendo wa siku tatu jangwani, ili tumtolee dhabihu BWANA Mungu wetu.


nitawajia kama dubu aliyenyang'anywa watoto wake; nami nitararua nyama ya mioyo yao; na huko nitawala kama simba; huyo mnyama mkali atawararua.


Ndipo Musa akamwambia Haruni, Jambo hili ni hilo BWANA alilolinena, akisema, Nitatakaswa mimi katika hao wanikaribiao, nami nitatukuzwa mbele ya watu hao wote. Haruni akanyamaza kimya.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo