Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Kutoka 39:43 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

43 Musa akaiona hiyo kazi yote, na tazama, walikuwa wameimaliza; vile vile kama BWANA alivyoagiza, walikuwa wameifanya vivyo hivyo; basi Musa akawaombea heri.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

43 Mose alikagua kila kitu, akaridhika kwamba walikuwa wamefanya kila kitu kama Mwenyezi-Mungu alivyoamuru. Hivyo Mose akawabariki.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

43 Mose alikagua kila kitu, akaridhika kwamba walikuwa wamefanya kila kitu kama Mwenyezi-Mungu alivyoamuru. Hivyo Mose akawabariki.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

43 Mose alikagua kila kitu, akaridhika kwamba walikuwa wamefanya kila kitu kama Mwenyezi-Mungu alivyoamuru. Hivyo Mose akawabariki.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

43 Musa akakagua kazi na kuona kuwa walikuwa wameifanya sawasawa na jinsi Mwenyezi Mungu alivyokuwa ameagiza. Kwa hiyo Musa akawabariki.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

43 Musa akakagua kazi na kuona kuwa walikuwa wameifanya sawasawa kama vile bwana alivyokuwa ameagiza. Kwa hiyo Musa akawabariki.

Tazama sura Nakili




Kutoka 39:43
24 Marejeleo ya Msalaba  

Mungu akaona kila kitu alichokifanya, na tazama, ni chema sana. Ikawa jioni ikawa asubuhi, siku ya sita.


Akambariki, akasema, Abramu na abarikiwe na Mungu Aliye Juu Sana, Muumba mbingu na nchi.


Kisha Daudi alipokwisha kutoa sadaka ya kuteketezwa na sadaka za amani akawabariki watu kwa jina la BWANA wa majeshi.


Na katika mwaka wa kumi na mmoja, katika mwezi wa Buli, ndio mwezi wa nane, nyumba ikaisha, mambo yake yote, kulingana na kanuni zote. Basi muda wa miaka saba alikuwa katika kuijenga.


Mfalme akageuza uso wake, akawabariki mkutano wote wa Israeli; na mkutano wote wa Israeli wakasimama.


Akasimama, na kuwabariki mkutano wote wa Israeli kwa sauti kuu, akasema,


Na Daudi alipokwisha kuitoa sadaka ya kuteketezwa na sadaka za amani, akawabariki watu kwa jina la BWANA.


Ndipo wakasimama makuhani Walawi, wakawabariki watu; ikasikiwa sauti yao, sala yao ikafika hata makao yake matakatifu, yaani, mbinguni.


Mfalme akageukia mkutano wote wa Israeli akawabariki, mkutano wote wa Israeli ukiwa umesimama.


Na hao watu wakawabariki wote waliojitoa kwa hiari wakae Yerusalemu.


Utukufu wa BWANA na udumu milele; BWANA na ayafurahie matendo yake.


Tena mtumishi wako huonywa kwazo, Katika kuzishika kuna thawabu kuu.


Basi wana wa Israeli wakaenda na kufanya mambo hayo; vile vile kama BWANA alivyowaamuru Musa na Haruni, ndivyo walivyofanya.


Sawasawa na haya yote nikuoneshayo, mfano wa maskani, na mfano wa samani zake zote, ndivyo mtakavyovifanya.


Sawasawa na yote BWANA aliyomwagiza Musa, ndivyo walivyoifanya hiyo kazi yote wana wa Israeli.


BWANA akanena na Musa, na kumwambia,


Kisha akaziwasha taa zake mbele za BWANA, kama BWANA alivyomwamuru Musa.


Musa na Haruni wakafanya vivyo hivyo; kama BWANA alivyowaambia, ndivyo walivyofanya.


Basi nikaenda, nikakificha karibu na mto Frati, kama BWANA alivyoniamuru.


Na amri hii itakuwa amri ya milele kwenu, ili kufanya upatanisho kwa ajili ya wana wa Israeli kwa sababu ya dhambi zao zote, mara moja kila mwaka. Naye akafanya vile vile kama BWANA alivyomwamuru Musa.


Basi Yoshua akawabariki, na kuwapa ruhusa waende zao; nao wakaenda mahemani kwao.


Basi Musa alikuwa amewapa hiyo nusu moja ya kabila la Manase urithi katika Bashani; lakini hiyo nusu ya pili Yoshua aliwapa urithi kati ya ndugu zao, ng'ambo ya Yordani upande wa kuelekea magharibi. Zaidi ya hayo Yoshua, hapo alipowaruhusu waende zao mahemani kwao, akawabariki,


Tufuate:

Matangazo


Matangazo