Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Kutoka 39:42 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

42 Sawasawa na yote BWANA aliyomwagiza Musa, ndivyo walivyoifanya hiyo kazi yote wana wa Israeli.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

42 Waisraeli walifanya kila kitu kama Mwenyezi-Mungu alivyomwamuru Mose.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

42 Waisraeli walifanya kila kitu kama Mwenyezi-Mungu alivyomwamuru Mose.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

42 Waisraeli walifanya kila kitu kama Mwenyezi-Mungu alivyomwamuru Mose.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

42 Waisraeli walikuwa wamefanya kazi yote sawasawa na vile Mwenyezi Mungu alivyokuwa amemwagiza Musa.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

42 Waisraeli walikuwa wamefanya kazi yote sawasawa na vile bwana alivyokuwa amemwagiza Musa.

Tazama sura Nakili




Kutoka 39:42
15 Marejeleo ya Msalaba  

Na katika mwaka wa kumi na mmoja, katika mwezi wa Buli, ndio mwezi wa nane, nyumba ikaisha, mambo yake yote, kulingana na kanuni zote. Basi muda wa miaka saba alikuwa katika kuijenga.


Wala hawakuyaacha maagizo ya mfalme aliyowaamuru makuhani na Walawi kwa neno lolote, wala kwa habari ya hazina.


Basi wana wa Israeli wakaenda na kufanya mambo hayo; vile vile kama BWANA alivyowaamuru Musa na Haruni, ndivyo walivyofanya.


Na kila mtu kati yenu aliye na moyo wa hekima na aje, na kuyafanya hayo yote ambayo BWANA ameyaagiza;


Basi ndivyo ilivyomalizwa kazi yote ya maskani ya hema ya kukutania; na wana wa Israeli walifanya kama yote BWANA aliyomwagiza Musa, ndivyo walivyofanya.


na mavazi ya kazi nzuri kwa utumishi katika mahali patakatifu, na mavazi matakatifu ya Haruni kuhani, na mavazi ya wanawe, ili kutumika katika kazi ya ukuhani.


Musa akaiona hiyo kazi yote, na tazama, walikuwa wameimaliza; vile vile kama BWANA alivyoagiza, walikuwa wameifanya vivyo hivyo; basi Musa akawaombea heri.


Basi nikaenda, nikakificha karibu na mto Frati, kama BWANA alivyoniamuru.


Ikiwa lile wingu lilikawia, likikaa juu ya maskani siku mbili, au mwezi, au mwaka, wana wa Israeli walikaa katika kambi yao, wasisafiri;


na kuwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru ninyi; na tazama, mimi nipo pamoja nanyi siku zote, hata ukamilifu wa dahari.


Neno lolote ninalowaagiza lizingatieni, usilizidishe, wala usilipunguze.


Jitahidi kujionesha kuwa umekubaliwa na Mungu, mfanyakazi asiye na sababu ya kutahayari, ukitumia kwa halali neno la kweli.


Nimevipiga vita vilivyo vizuri, mwendo nimeumaliza, Imani nimeilinda;


Tufuate:

Matangazo


Matangazo