Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Kutoka 38:27 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

27 Na hizo talanta mia moja za fedha zilikuwa kwa kutengenezea vile vitako vya mahali patakatifu na vitako vya hilo pazia; vitako mia moja kwa hizo talanta mia moja, talanta moja kitako kimoja.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

27 Kilo 3,000 za fedha zilitumika kutengenezea vile vikalio 100 vya hema takatifu na lile pazia, yaani kilo 30 kwa kila kikalio.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

27 Kilo 3,000 za fedha zilitumika kutengenezea vile vikalio 100 vya hema takatifu na lile pazia, yaani kilo 30 kwa kila kikalio.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

27 Kilo 3,000 za fedha zilitumika kutengenezea vile vikalio 100 vya hema takatifu na lile pazia, yaani kilo 30 kwa kila kikalio.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

27 Talanta hizo mia moja za fedha zilitumika kusubu vile vitako mia moja kwa ajili ya mahali patakatifu na pazia: vitako mia moja kwa talanta mia, yaani talanta moja kwa kila kitako.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

27 Talanta hizo 100 za fedha zilitumika kusubu vile vitako mia moja kwa ajili ya mahali patakatifu na pazia: vitako mia moja kwa talanta mia, yaani, talanta moja kwa kila kitako.

Tazama sura Nakili




Kutoka 38:27
6 Marejeleo ya Msalaba  

Nawe ufanye vitako arubaini vya fedha chini ya zile mbao ishirini, vitako viwili chini ya ubao mmoja, kupokea zile ndimi zake mbili, na vitako viwili chini ya ubao mwingine kupokea zile ndimi zake mbili;


na vitako vyake vya fedha arubaini; vitako viwili chini ya ubao mmoja, na vitako viwili chini ya ubao mwingine.


Mbao zitakuwa ni nane, na vitako vyake vya fedha, vitako kumi na sita; vitako viwili chini ya ubao mmoja, na vitako viwili chini ya ubao wa pili.


kisha litungike katika nguzo nne za mti wa mshita zilizofunikwa dhahabu, vifungo vyake vitakuwa vya dhahabu, katika vitako vya fedha vinne.


kichwa beka, maana, nusu shekeli, kwa kadiri ya shekeli ya mahali patakatifu, kwa ajili ya kila mtu aliyepita kwa wale waliohesabiwa, aliyekuwa wa umri wa miaka ishirini au zaidi, kwa ajili ya wanaume elfu mia sita na tatu mia tano na hamsini (603,550).


Na kwa hizo shekeli elfu moja na mia saba, na sabini na tano, akafanya vifungo vya hizo nguzo, na kuvifunika fedha vile vichwa vyake, na kufanya vitanzi vyake.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo