Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Kutoka 38:25 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

25 Na fedha ya hao waliohesabiwa, watu wa huo mkutano ilikuwa talanta mia moja, na shekeli elfu moja na mia saba na sabini na tano kwa kadiri ya shekeli ya mahali patakatifu;

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

25 Fedha waliyochanga hao watu wa jumuiya waliohesabiwa ilikuwa ya uzito wa kilo 3,017 na gramu 750 kulingana na vipimo vya hema takatifu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

25 Fedha waliyochanga hao watu wa jumuiya waliohesabiwa ilikuwa ya uzito wa kilo 3,017 na gramu 750 kulingana na vipimo vya hema takatifu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

25 Fedha waliyochanga hao watu wa jumuiya waliohesabiwa ilikuwa ya uzito wa kilo 3,017 na gramu 750 kulingana na vipimo vya hema takatifu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

25 Fedha iliyopatikana kutokana na jumuiya ya watu waliohesabiwa ilikuwa yenye uzito wa talanta mia moja na shekeli elfu moja mia saba sabini na tano (1,775), kulingana na shekeli ya mahali patakatifu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

25 Fedha iliyopatikana kutokana na jumuiya ya watu waliohesabiwa ilikuwa yenye uzito wa talanta mia moja na shekeli 1,775, kulingana na shekeli ya mahali patakatifu.

Tazama sura Nakili




Kutoka 38:25
5 Marejeleo ya Msalaba  

BWANA akanena na Musa, na kumwambia,


Utakapowahesabu wana wa Israeli, kama itakavyotokea hesabu yao, ndipo watakapompa BWANA kila mtu ukombozi kwa ajili ya roho yake, hapo utakapowahesabu; ili kwamba yasiwe maradhi kati yao, hapo utakapowahesabu.


Nawe utapokea hizo fedha za upatanisho mikononi mwa hao wana wa Israeli, na kuziweka kwa ajili ya utumishi wa hema ya kukutania; ili kwamba ziwe ukumbusho kwa ajili ya wana wa Israeli mbele ya BWANA, ili kufanya upatanisho kwa ajili ya roho zenu.


Fanyeni hesabu ya watu wote wa Israeli, kwa kufuata jamaa zao, na nyumba za baba zao, kama hesabu ya majina ilivyo, kila mwanamume mmoja mmoja;


Fanya hesabu ya jumuiya yote ya wana wa Israeli, tangu umri wa miaka ishirini, na zaidi, kwa nyumba za baba zao, hao wote katika Israeli wawezao kutoka kuenenda vitani.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo