Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Kutoka 35:35 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

35 Amewajaza watu hao ujuzi, ili watumike katika kazi za kila aina, mawe, na kazi ya fundi mwenye kutia taraza, katika nyuzi za rangi ya buluu, zambarau na nyekundu, na kitani nzuri, ya mwenye kufuma nguo; ya hao wafanyao kazi yoyote, na ya wenye kuvumbua kazi za werevu.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

35 Amewapa ujuzi wa kufanya kila kazi ya ufundi au ifanywayo na watu wa sanaa au mafundi wa kutarizi kwa sufu ya rangi ya buluu, zambarau na nyekundu na kitani safi iliyosokotwa, kwa kutumia ufundi wowote wa msanii.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

35 Amewapa ujuzi wa kufanya kila kazi ya ufundi au ifanywayo na watu wa sanaa au mafundi wa kutarizi kwa sufu ya rangi ya buluu, zambarau na nyekundu na kitani safi iliyosokotwa, kwa kutumia ufundi wowote wa msanii.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

35 Amewapa ujuzi wa kufanya kila kazi ya ufundi au ifanywayo na watu wa sanaa au mafundi wa kutarizi kwa sufu ya rangi ya buluu, zambarau na nyekundu na kitani safi iliyosokotwa, kwa kutumia ufundi wowote wa msanii.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

35 Amewajaza ustadi wa kufanya kazi za aina zote zinazofanywa na mafundi, na wenye kubuni michoro, pia na watarizi kwa rangi za buluu, zambarau, nyekundu na kitani safi, na wafumaji: wote wakiwa mafundi na wabunifu hodari.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

35 Amewajaza ustadi wa kufanya kazi za aina zote zifanywazo na mafundi, na wenye kubuni michoro, pia na watarizi kwa rangi za buluu, zambarau, nyekundu na kitani safi, na wafumaji: wote wakiwa mafundi na wabunifu hodari.

Tazama sura Nakili




Kutoka 35:35
23 Marejeleo ya Msalaba  

basi, tazama, nimefanya kama ulivyosema. Tazama, nimekupa moyo wa hekima na wa akili; hata kabla yako hapakuwa na mtu kama wewe, wala baada yako hatainuka mtu kama wewe.


Naye alikuwa mwana wa mwanamke mjane wa kabila la Naftali, na babaye alikuwa mtu wa Tiro, mfua shaba; naye alikuwa mwingi wa hekima na akili, stadi wa kufanya kazi zote za shaba. Akamfikia mfalme Sulemani, akamfanyia kazi yake yote.


mwana wa mwanamke wa kabila la Dani, na babaye alikuwa mkazi wa Tiro, yeye ni bingwa wa kutumia dhahabu, fedha, shaba, chuma, mawe na mti; na wa nguo za urujuani, samawati, nyekundu na kitani safi; tena ni stadi kwa kutia nakshi na kuchora michoro yoyote, mbunifu na kuchora chochote kufuatana na kielekezo ambacho angepewa yeye na watu wako mastadi wa bwana wangu Daudi baba yako.


Siku zangu hupita upesi kuliko chombo cha kufumia, Nazo zapita pasipokuwa na matumaini.


Kisha fanya hiyo maskani iwe na mapazia kumi; ifanye ya nguo ya kitani nzuri ya kusokota, pamoja na nyuzi za rangi ya buluu, zambarau na nyekundu, pamoja na makerubi; kazi ya fundi stadi.


nami nimemjaza Roho ya Mungu, katika hekima, na maarifa, na ujuzi, na mambo ya kazi ya kila aina,


Tena, tazama, nimemchagua, awe pamoja naye, huyo Oholiabu, mwana wa Ahisamaki, wa kabila la Dani; nami nimetia hekima katika mioyo ya wote wenye moyo wa hekima, ili wapate kutengeneza vyote nilivyokuagiza;


naye amemjaza Roho ya Mungu, katika hekima, na akili, na ujuzi, na kazi ya ustadi kila aina;


Basi Bezaleli na Oholiabu watatenda kazi, na kila mtu mwenye moyo wa hekima, ambaye BWANA amemtia akili na hekima ili ajue kufanya kazi hiyo yote kwa huo utumishi wa mahali patakatifu, kama hayo yote BWANA aliyoyaagiza.


Kwa maana Mungu wake anamwagiza vizuri na kumfundisha.


Makao yangu yameondolewa kabisa, yamechukuliwa kama hema ya mchungaji; Nimekunja maisha yangu kama mfumaji; atanikatilia mbali na kitanda cha mfumi; Tangu mchana hata usiku wanimaliza.


Na Paulo, alipokwisha kuweka mikono yake juu yao, Roho Mtakatifu akaja juu yao; wakaanza kunena kwa lugha, na kutabiri.


Akaingia ndani ya sinagogi, akanena kwa ushujaa kwa muda wa miezi mitatu, akihojiana na watu, na kuwavuta katika mambo ya ufalme wa Mungu.


kwa kuwa katika kila jambo mlitajirika katika yeye, katika maneno yote, na maarifa yote;


hata hamkupungukiwa na karama yoyote, mkikutazamia sana kufunuliwa kwake Bwana wetu Yesu Kristo;


Maana kama vile mwili ni mmoja, nao una viungo vingi, na viungo vyote vya mwili ule, navyo ni vingi, ni mwili mmoja; vivyo hivyo na Kristo.


Basi kuna karama tofauti; bali Roho ni yeye yule.


Maana mtu mmoja kwa Roho apewa neno la hekima; na mwingine neno la maarifa, apendavyo Roho yeye yule;


Nataka kujifunza neno hili moja kwenu. Je! Mlipokea Roho kwa matendo ya sheria, au kwa kusikia kunakotokana na imani?


Basi, yeye awapaye Roho na kufanya miujiza kati yenu, je! Afanya hayo kwa matendo ya sheria, au kwa kusikia kunakotokana na imani?


Lakini nikikawia, upate kujua jinsi iwapasavyo watu kuenenda katika nyumba ya Mungu, iliyo kanisa la Mungu aliye hai, nguzo na msingi wa kweli.


Jitunze nafsi yako, na mafundisho yako. Dumu katika mambo hayo; maana kwa kufanya hivyo utajiokoa nafsi yako, na wale wakusikiao pia.


Jitahidi kujionesha kuwa umekubaliwa na Mungu, mfanyakazi asiye na sababu ya kutahayari, ukitumia kwa halali neno la kweli.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo