Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Kutoka 35:22 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

22 Nao wakaja, wanaume kwa wanawake, wote waliokuwa na moyo wa kupenda, wakaleta vipini, hazama, pete za mhuri, vikuku na vyombo vyote vya dhahabu; kila mtu aliyetoa toleo la dhahabu la kumpa BWANA.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

22 Hivyo wote wenye moyo mkarimu, wanaume kwa wanawake, wakaleta vipini, pete za mhuri, vikuku na kila aina ya vyombo vya dhahabu; kila mtu akamtolea Mwenyezi-Mungu kitu cha dhahabu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

22 Hivyo wote wenye moyo mkarimu, wanaume kwa wanawake, wakaleta vipini, pete za mhuri, vikuku na kila aina ya vyombo vya dhahabu; kila mtu akamtolea Mwenyezi-Mungu kitu cha dhahabu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

22 Hivyo wote wenye moyo mkarimu, wanaume kwa wanawake, wakaleta vipini, pete za mhuri, vikuku na kila aina ya vyombo vya dhahabu; kila mtu akamtolea Mwenyezi-Mungu kitu cha dhahabu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

22 Wote waliopenda, wanaume na wanawake, wakaja wakaleta vito vya dhahabu vya kila aina: vipini, vipuli, pete na mapambo. Wote wakatoa dhahabu zao kuwa sadaka ya kuinuliwa kwa Mwenyezi Mungu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

22 Wote waliokuwa na utayari, wanaume kwa wanawake, wakaja wakaleta vito vya dhahabu vya kila aina: vipini, vipuli, pete na mapambo. Wote wakatoa dhahabu zao kama sadaka ya kuinuliwa kwa bwana.

Tazama sura Nakili




Kutoka 35:22
18 Marejeleo ya Msalaba  

Yoashi akawaambia makuhani, Fedha yote ya vitu vitakatifu iliyoletwa nyumbani mwa BWANA, fedha ya matumizi, fedha ya watu kadiri alivyoandikiwa kila mtu, na fedha yote iliyoletwa kama mtu yeyote aonavyo moyoni mwake kuileta nyumbani mwa BWANA,


Ndipo Hezekia akajibu, akasema, Sasa mmejifanya wakfu kwa BWANA, karibuni mkalete dhabihu na matoleo ya shukrani nyumbani mwa BWANA. Basi kusanyiko wakaleta dhabihu na matoleo ya shukrani; na wote wenye moyo wa ukarimu, wakaleta sadaka za kuteketezwa.


Haruni akawaambia, Zivunjeni pete za dhahabu zilizo katika masikio ya wake zenu, na wana wenu, na binti zenu, mniletee.


Watu wote wakazivunja pete za dhahabu zilizo katika masikio yao, wakamletea Haruni.


Wakaja kila mtu ambaye moyo wake ulimhimiza, na kila mtu ambaye roho yake ilimfanya kuwa apenda, nao wakaleta sadaka za kumpa BWANA, kwa kazi ya hema ya kukutania, na kwa utumishi wake, na kwa hayo mavazi matakatifu.


Tena kila mtu aliyeona kwake nyuzi za rangi ya buluu, zambarau na nyekundu, na kitani nzuri, singa za mbuzi, ngozi za kondoo dume zilizotiwa rangi nyekundu na ngozi za pomboo, akavileta.


Kipuli cha dhahabu, na pambo la dhahabu safi; Ndivyo alivyo mwonyaji mwenye hekima kwa sikio lisikialo.


na pete za masikio, na vikuku, na mataji yao;


Utukufu wa Lebanoni utakujia wewe, Mberoshi na mtidhari na mteashuri pamoja; Ili kupapamba mahali pangu patakatifu, Nami nitapatukuza mahali pa miguu yangu.


Hakika yake visiwa vitaningojea, Na merikebu za Tarshishi kwanza, Ili kuleta wana wako kutoka mbali, Na fedha yao na dhahabu yao pamoja nao, Kwa ajili ya jina la BWANA, Mungu wako, Kwa ajili yake Mtakatifu wa Israeli, Kwa kuwa amekutukuza wewe.


Nikakupamba kwa mapambo pia, nikatia vikuku mikononi mwako, na mkufu shingoni mwako.


Nasi tumeleta matoleo ya BWANA, aliyopata kila mtu, ya vyombo vya dhahabu, na mitali, na timbi, na pete za mhuri, na vipini, na vikuku, ili kuzifanyia upatanisho nafsi zetu mbele ya BWANA.


Wakaingia nyumbani, wakamwona mtoto pamoja na Mariamu mamaye, wakaanguka wakamsujudia; nao walipokwisha kufungua hazina zao, wakamtolea tunu; dhahabu, uvumba na manemane.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo