Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Kutoka 35:21 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

21 Wakaja kila mtu ambaye moyo wake ulimhimiza, na kila mtu ambaye roho yake ilimfanya kuwa apenda, nao wakaleta sadaka za kumpa BWANA, kwa kazi ya hema ya kukutania, na kwa utumishi wake, na kwa hayo mavazi matakatifu.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

21 Kila mtu aliyevutwa na kusukumwa moyoni mwake alimtolea Mungu mchango wake kwa ajili ya hema la mkutano, huduma zake zote na mavazi yake matakatifu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

21 Kila mtu aliyevutwa na kusukumwa moyoni mwake alimtolea Mungu mchango wake kwa ajili ya hema la mkutano, huduma zake zote na mavazi yake matakatifu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

21 Kila mtu aliyevutwa na kusukumwa moyoni mwake alimtolea Mungu mchango wake kwa ajili ya hema la mkutano, huduma zake zote na mavazi yake matakatifu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

21 na kila mmoja aliyependa na ambaye moyo wake ulimsukuma alikuja na kuleta sadaka kwa Mwenyezi Mungu, kwa ajili ya kazi katika Hema la Kukutania, kwa ajili ya huduma yake yote na kwa ajili ya mavazi matakatifu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

21 na kila mmoja aliyependa na ambaye moyo wake ulimsukuma alikuja na kuleta sadaka kwa bwana, kwa ajili ya kazi katika Hema la Kukutania, kwa ajili ya huduma yake yote na kwa ajili ya mavazi matakatifu.

Tazama sura Nakili




Kutoka 35:21
28 Marejeleo ya Msalaba  

Kwa kuwa wewe, BWANA wa majeshi, Mungu wa Israeli umenifunulia mimi, mtumishi wako, ukisema, Nitakujengea nyumba; kwa hiyo mimi, mtumishi wako, nimepata ujasiri nikuombe ombi hili.


Ndipo Daudi mfalme akasimama kwa miguu yake, akasema, Nisikilizeni, ndugu zangu, na watu wangu; Mimi nilikuwa na nia ya kuijenga nyumba ya kuliweka sanduku la Agano la BWANA, na kiti cha kuwekea miguu cha Mungu wetu; hata nilikuwa nimejitayarisha kujenga.


Nawe, Sulemani mwanangu, mjue Mungu wa baba yako, ukamtumikie kwa moyo mkamilifu, na kwa nia ya kumkubali; kwa kuwa BWANA huchunguza mioyo yote, na kuyatambua mawazo yote ya fikira; ukimtafuta, atakuwa nawe; ukimwacha, atakutupa milele.


Lakini mimi ni nani, na watu wangu ni nani, hata tuweze kutoa kwa hiari hivi? Kwani vitu vyote vyatoka kwako na katika vitu vyako mwenyewe tumekutolea.


Nami tena kwa kuwa nimeiwekea nyumba ya Mungu wangu shauku yangu, nami ninayo hazina yangu mwenyewe ya dhahabu na fedha, ninaitoa kwa ajili ya nyumba ya Mungu wangu, zaidi ya hiyo akiba niliyoiwekea tayari nyumba takatifu;


Na wale walioonekana kuwa na vito vya thamani wakavitoa vitiwe katika hazina ya nyumba ya BWANA, chini ya mkono wa Yehieli, Mgershoni.


Ndipo hao watu wakafurahi, kwa sababu wametoa kwa hiari yao wenyewe, kwa moyo wao wote, kwa hiari yao wenyewe, wamemtolea BWANA; mfalme Daudi naye akafurahi sana.


Na baadhi ya wakuu wa koo za baba zao, hapo walipoifikia nyumba ya BWANA, iliyoko Yerusalemu, walitoa mali kwa ukarimu kwa ajili ya nyumba ya Mungu, ili kuisimamisha mahali pake;


Na ahimidiwe BWANA, Mungu wa baba zetu, aliyetia neno kama hilo katika moyo wa mfalme, kuipamba nyumba ya BWANA iliyoko Yerusalemu.


Watu wako watajitoa kwa hiari, Siku ya uwezo wako; Kwa uzuri wa utakatifu, Tokea tumbo la asubuhi, Unao umande wa ujana wako.


Waambie wana wa Israeli kwamba wanitwalie sadaka; kila mtu ambaye moyo wake wampa kupenda mtatwaa kwake sadaka yangu.


Basi mkutano wote wa wana wa Israeli wakaondoka hapo mbele ya Musa.


Nao wakaja, wanaume kwa wanawake, wote waliokuwa na moyo wa kupenda, wakaleta vipini, hazama, pete za mhuri, vikuku na vyombo vyote vya dhahabu; kila mtu aliyetoa toleo la dhahabu la kumpa BWANA.


Na wanawake wote ambao mioyo yao iliwahimiza katika hekima wakasokota hizo singa za mbuzi.


Wana wa Israeli wakaleta sadaka za kumpa BWANA kwa moyo wa kupenda; wote, wanaume kwa wanawake, ambao mioyo yao iliwafanya kuwa wapenda kuleta kwa hiyo kazi, ambayo BWANA aliamuru ifanywe kwa mkono wa Musa.


Katwaeni kati yenu matoleo kwa BWANA; mtu yeyote aliye na moyo wa kupenda, ayalete matoleo; dhahabu na fedha na shaba;


Basi Musa akawaita Bezaleli na Oholiabu, na kila mtu aliyekuwa na moyo wa akili, ambaye BWANA alimtia moyoni mwake hekima, kila mtu ambaye moyo wake ulimhimiza ili aende kuifanya kazi hiyo;


Linda moyo wako kuliko yote uyalindayo; Maana ndiko zitokako chemchemi za uzima.


Na mkuu wao atakuwa mtu wa kwao wenyewe, naye mwenye kuwatawala atakuwa mtu wa jamaa yao; nami nitamkaribisha, naye atanikaribia; maana ni nani aliye na moyo wa kuthubutu kunikaribia? Asema BWANA.


Enyi wazawa wa nyoka, mwawezaje kunena mema, mkiwa wabaya? Maana, kinywa cha mtu huyanena yaujazayo moyo wake.


Maana, kama nia ipo, hukubaliwa kwa kadiri ya alivyo navyo mtu, si kwa kadiri ya asivyo navyo.


Kila mtu na atende kama alivyokusudia moyoni mwake, si kwa huzuni, wala si kwa lazima; maana Mungu humpenda yeye atoaye kwa moyo mkunjufu.


Amka, amka, Debora; Amka, amka, imba wimbo. Inuka, Baraka, wachukue mateka wao Waliokuchukua mateka, Ee mwana wa Abinoamu.


Sikieni, enyi wafalme; tegeni masikio, enyi wakuu; Mimi, naam mimi, nitamwimbia BWANA; Nitamhimidi BWANA, Mungu wa Israeli.


Moyo wangu unawaelekea makamanda wa Israeli, Waliojitoa nafsi zao kwa hiari yao miongoni mwa watu; Mhimidini BWANA.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo