Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Kutoka 34:2 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

2 Nawe uwe tayari asubuhi, ukwee juu katika mlima wa Sinai asubuhi, nawe leta nafsi yako kwangu huko katika kilele cha mlima.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

2 Uwe tayari kesho asubuhi, uje kukutana nami mlimani Sinai.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

2 Uwe tayari kesho asubuhi, uje kukutana nami mlimani Sinai.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

2 Uwe tayari kesho asubuhi, uje kukutana nami mlimani Sinai.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

2 Uwe tayari asubuhi, kisha upande juu ya Mlima Sinai. Uje mbele zangu kukutana nami huko juu ya mlima.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

2 Uwe tayari asubuhi, kisha upande juu ya Mlima Sinai. Uje mbele zangu kukutana nami huko juu ya mlima.

Tazama sura Nakili




Kutoka 34:2
6 Marejeleo ya Msalaba  

wawe tayari kwa siku ya tatu; maana siku ya tatu BWANA atashuka katika mlima wa Sinai machoni pa watu hawa wote.


Mlima wa Sinai wote pia ukatoa moshi, kwa sababu BWANA alishuka katika moto; na ule moshi wake ukapanda juu kama moshi wa tanuri, mlima wote ukatetemeka sana.


BWANA akaushukia mlima, juu ya kilele cha mlima; BWANA akamwita Musa aende hata kilele cha mlima; Musa akapanda juu.


BWANA akamwambia, Nenda, ushuke wewe; nawe utakwea, wewe, na Haruni pamoja nawe; lakini wale makuhani na watu wasipenye kumkaribia BWANA, asije yeye akawafurikia juu yao.


BWANA akamwambia Musa, Njoo huku juu kwangu mlimani, uwe huku; nami nitakupa vibao vya mawe na ile sheria na hiyo amri niliyoiandika ili uwafundishe.


Ndipo nikaanguka chini mbele za BWANA siku zile arubaini usiku na mchana nilizokuwa nimeanguka chini; kwa kuwa BWANA alisema atawaangamiza.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo