Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Kutoka 33:7 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

7 Basi desturi ya Musa, ilikuwa kuitwaa ile hema, na kuikita nje ya kambi na mbali hiyo kambi; akaiita, hema ya kukutania. Hata kila mtu aliyekuwa akitaka neno kwa BWANA, akatoka, akaenda hata hema ya kukutania, iliyokuwa nje ya kambi.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

7 Mose alikuwa na desturi ya kulichukua lile hema na kulisimika nje ya kambi. Hema hilo alilipa jina, Hema la Mkutano. Mtu yeyote aliyetaka shauri kwa Mwenyezi-Mungu alikwenda kwenye hema la mkutano nje ya kambi.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

7 Mose alikuwa na desturi ya kulichukua lile hema na kulisimika nje ya kambi. Hema hilo alilipa jina, Hema la Mkutano. Mtu yeyote aliyetaka shauri kwa Mwenyezi-Mungu alikwenda kwenye hema la mkutano nje ya kambi.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

7 Mose alikuwa na desturi ya kulichukua lile hema na kulisimika nje ya kambi. Hema hilo alilipa jina, Hema la Mkutano. Mtu yeyote aliyetaka shauri kwa Mwenyezi-Mungu alikwenda kwenye hema la mkutano nje ya kambi.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

7 Basi Musa alikuwa na desturi ya kuchukua hema na kuliweka wakfu nje ya kambi umbali kiasi, akaliita “Hema la Kukutania”. Kila aliyekuwa akiulizia shauri kwa Mwenyezi Mungu, angeenda hadi Hema la Kukutania, nje ya kambi.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

7 Basi Musa alikuwa na desturi ya kuchukua hema na kuliweka wakfu nje ya kambi umbali kiasi, akaliita “Hema la Kukutania.” Kila aliyekuwa akiulizia shauri kwa bwana, angelikwenda katika Hema la Kukutania nje ya kambi.

Tazama sura Nakili




Kutoka 33:7
17 Marejeleo ya Msalaba  

Kulikuwa na njaa siku za Daudi muda wa miaka mitatu, mwaka kwa mwaka; naye Daudi akautafuta uso wa BWANA. BWANA akasema, Ni kwa ajili ya Sauli, na kwa nyumba yake yenye damu, kwa kuwa aliwaua hao Wagibeoni.


Ee BWANA, kwa nini wasimama mbali? Kwani unajificha nyakati za shida?


Uliposema, “Nitafuteni uso wangu,” Moyo wangu umekuambia, BWANA, uso wako nitautafuta.


Wewe, BWANA, umeona, usinyamaze; Ee Bwana, usiwe mbali nami.


Yethro mkwewe Musa akamletea Mungu sadaka ya kuteketezwa na dhabihu; na Haruni akaja, na wazee wote wa Israeli, wale chakula pamoja na mkwewe Musa mbele za Mungu.


Basi Musa akatoka nje ili amlaki mkwewe, akasujudia na kumbusu; nao wakaulizana habari; kisha wakaingia hemani.


Basi wana wa Israeli wakavua mapambo yao, tangu mlima wa Horebu na mbele.


Hata Musa alipotoka kuiendea ile hema, watu wote waliondoka wakasimama, kila mtu mlangoni pa hema yake, akamtazama Musa, hata alipokwisha kuingia hemani.


BWANA yuko mbali na wasio haki; Bali huisikia sala ya mwenye haki.


lakini maovu yenu yamewafarikisha ninyi na Mungu wenu, na dhambi zenu zimeuficha uso wake msiuone, hata hataki kusikia.


Wajapolea watoto wao, mimi nitawanyang'anya watoto wao, asisalie hata mtu mmoja; naam, ole wao! Nitakapoondoka na kuwaacha.


Lakini huko, kama mkimtafuta BWANA, Mungu wako, utampata, ukimtafuta kwa moyo wako wote, na roho yako yote.


mhudumu wa patakatifu, na wa ile hema ya kweli, ambayo Bwana aliiweka wala si mwanadamu.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo