Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Kutoka 32:29 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

29 Musa akasema, Jiwekeni wakfu kwa BWANA leo, kila mtu juu ya mwanawe na juu ya ndugu yake; ili awape baraka leo.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

29 Mose akasema, “Leo mmejiweka wakfu nyinyi wenyewe kumhudumia Mwenyezi-Mungu, kwa vile hamkusita hata kuwaua watoto wenu au ndugu zenu. Mungu awajalie baraka leo hii.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

29 Mose akasema, “Leo mmejiweka wakfu nyinyi wenyewe kumhudumia Mwenyezi-Mungu, kwa vile hamkusita hata kuwaua watoto wenu au ndugu zenu. Mungu awajalie baraka leo hii.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

29 Mose akasema, “Leo mmejiweka wakfu nyinyi wenyewe kumhudumia Mwenyezi-Mungu, kwa vile hamkusita hata kuwaua watoto wenu au ndugu zenu. Mungu awajalie baraka leo hii.”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

29 Kisha Musa akasema, “Leo mmewekwa wakfu kwa Mwenyezi Mungu, kwa kuwa mlikuwa kinyume na wana wenu wenyewe na ndugu zenu, naye Mungu amewabariki leo.”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

29 Kisha Musa akasema, “Leo mmewekwa wakfu kwa bwana, kwa kuwa mlikuwa kinyume na wana wenu wenyewe na ndugu zenu, naye Mungu amewabariki leo.”

Tazama sura Nakili




Kutoka 32:29
11 Marejeleo ya Msalaba  

Akawaambia Walawi, waliowafundisha Israeli wote, waliotakasika kwa BWANA, Wekeni sanduku takatifu katika nyumba aliyoijenga Sulemani, mwana wa Daudi, mfalme wa Israeli; hamtakuwa tena na mzigo mabegani; sasa mtumikieni BWANA, Mungu wenu, na watu wake Israeli.


Na hao wana wa Lawi wakafanya kama vile alivyosema Musa, wakaanguka siku ile kama watu elfu tatu.


Hata asubuhi yake Musa akawaambia watu, Mmetenda dhambi kuu; na sasa nitakwenda juu kwa BWANA, labda nitafanya upatanisho kwa ajili ya dhambi yenu.


Kutenda haki na hukumu Humpendeza BWANA kuliko kutoa sadaka.


Tena itakuwa ya kwamba, mtu awaye yote atakapotoa unabii, basi baba yake na mama yake waliomzaa watamwambia, Hutaishi; kwa maana unanena maneno ya uongo kwa jina la BWANA; na baba yake na mama yake waliomzaa watamtumbua atoapo unabii.


Apendaye baba au mama kuliko mimi, hanistahili; wala apendaye mwana au binti kuliko mimi, hanistahili.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo