Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Kutoka 31:2 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

2 Angalia, nimemwita kwa jina lake Bezaleli mwana wa Uri, mwana wa Huri, wa kabila la Yuda;

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

2 “Mimi nimemteua Bezaleli, mwana wa Uri, mjukuu wa Huri, wa kabila la Yuda

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

2 “Mimi nimemteua Bezaleli, mwana wa Uri, mjukuu wa Huri, wa kabila la Yuda

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

2 “Mimi nimemteua Bezaleli, mwana wa Uri, mjukuu wa Huri, wa kabila la Yuda

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

2 “Tazama, nimemchagua Bezaleli mwana wa Uri, mwana wa Huri, wa kabila la Yuda,

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

2 “Tazama, nimemchagua Bezaleli mwana wa Uri, mwana wa Huri, wa kabila la Yuda,

Tazama sura Nakili




Kutoka 31:2
14 Marejeleo ya Msalaba  

Naye alikuwa mwana wa mwanamke mjane wa kabila la Naftali, na babaye alikuwa mtu wa Tiro, mfua shaba; naye alikuwa mwingi wa hekima na akili, stadi wa kufanya kazi zote za shaba. Akamfikia mfalme Sulemani, akamfanyia kazi yake yote.


Tena madhabahu ya shaba, aliyoifanya Bezaleli mwana wa Uri, mwana wa Huri, ilikuwako huko mbele ya maskani ya BWANA; Sulemani na kusanyiko wakaiendea.


Basi Yoshua akafanya kama Musa alivyomwambia, akapigana na Amaleki; na Musa na Haruni na Huri wakapanda juu ya kile kilima.


Musa akamwambia BWANA, Angalia, wewe waniambia, Wachukue watu hawa; nawe hukunijulisha ni nani utakayemtuma pamoja nami. Lakini umesema, Nakujua jina lako, nawe umepata neema mbele zangu.


BWANA akamwambia Musa, Nitafanya na neno hili ulilolinena, kwa maana umepata neema mbele zangu, nami nakujua jina lako.


Kisha Musa akawaambia wana wa Israeli, Angalieni, BWANA amemwita kwa jina lake Bezaleli mwana wa Uri, mwana wa Huri, wa kabila la Yuda;


Basi Bezaleli na Oholiabu watatenda kazi, na kila mtu mwenye moyo wa hekima, ambaye BWANA amemtia akili na hekima ili ajue kufanya kazi hiyo yote kwa huo utumishi wa mahali patakatifu, kama hayo yote BWANA aliyoyaagiza.


Kisha Bezaleli akalifanya lile sanduku la mti wa mshita, urefu wake ulikuwa dhiraa mbili na nusu, na upana wake ulikuwa dhiraa moja na nusu, na kwenda juu kwake kulikuwa ni dhiraa moja na nusu;


Na Bezaleli mwana wa Uri, mwana wa Huri, wa kabila la Yuda, akafanya yote BWANA aliyomwagiza Musa.


Na pamoja naye alikuwa na Oholiabu, mwana wa Ahisamaki, wa kabila la Dani, aliyekuwa fundi wa kuchora nakshi, mfanyaji wa kazi mwerevu, naye alikuwa mwenye kutia taraza za nyuzi za rangi ya samawati, na za rangi ya zambarau, na nyekundu, na kitani nzuri.


Yohana akajibu, akasema, Hawezi mtu kupokea neno lolote isipokuwa amepewa kutoka mbinguni.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo