Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Kutoka 3:4 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

4 BWANA alipoona ya kuwa ameenda ili atazame, Mungu akamwita kutoka katikati ya kile kichaka, akasema, Musa! Musa! Akaitika, Mimi hapa.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

4 Mwenyezi-Mungu alipoona kwamba Mose amegeuka kukiangalia kichaka, akamwita pale kichakani, “Mose! Mose!” Mose akaitika, “Naam! Nasikiliza!”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

4 Mwenyezi-Mungu alipoona kwamba Mose amegeuka kukiangalia kichaka, akamwita pale kichakani, “Mose! Mose!” Mose akaitika, “Naam! Nasikiliza!”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

4 Mwenyezi-Mungu alipoona kwamba Mose amegeuka kukiangalia kichaka, akamwita pale kichakani, “Mose! Mose!” Mose akaitika, “Naam! Nasikiliza!”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

4 Mwenyezi Mungu alipoona kuwa amegeuka ili aone, Mungu akamwita kutoka ndani ya kile kichaka, “Musa! Musa!” Naye Musa akajibu, “Mimi hapa.”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

4 bwana alipoona kuwa amegeuka ili aone, Mungu akamwita kutoka ndani ya kile kichaka, “Musa! Musa!” Naye Musa akajibu, “Mimi hapa.”

Tazama sura Nakili




Kutoka 3:4
18 Marejeleo ya Msalaba  

Ikawa baada ya mambo hayo Mungu alimjaribu Abrahamu, akamwambia, Ee Abrahamu! Naye akasema, Mimi hapa.


Ndipo malaika wa BWANA akamwita kutoka mbinguni, akasema, Abrahamu! Abrahamu! Naye akasema, Mimi hapa.


Yakobo akaamka katika usingizi wake, akasema, Kweli BWANA yupo mahali hapa, ijapokuwa mimi sikujua.


Mungu akanena na Israeli katika ndoto ya usiku, akasema, Yakobo, Yakobo. Akasema, Mimi hapa.


Mara moja amenena Mungu; Mara mbili nimeyasikia haya, Ya kuwa nguvu zina Mungu,


Musa akapanda kwa Mungu, na BWANA akamwita kutoka mlimani ule, akisema, Utawaambia nyumba ya Yakobo, na kuwaarifu wana wa Israeli, maneno haya;


Malaika wa BWANA akamtokea, katika mwali wa moto uliotoka katikati ya kichaka; akatazama, na kumbe! Kile kichaka kiliwaka moto, nacho kichaka hakikuteketea.


Musa akamwambia BWANA, Angalia, wewe waniambia, Wachukue watu hawa; nawe hukunijulisha ni nani utakayemtuma pamoja nami. Lakini umesema, Nakujua jina lako, nawe umepata neema mbele zangu.


ili kwamba wapate kusadiki ya kwamba BWANA, Mungu wa Abrahamu, Mungu wa Isaka, Mungu wa Yakobo, amekutokea.


BWANA akamwita Musa, na kusema naye kutoka katika hema ya kukutania, akamwambia,


Kisha sauti ikamjia, kusema, Inuka, Petro, uchinje ule.


Akaona katika maono waziwazi, kama saa tisa ya mchana, malaika wa Mungu, akimjia na kumwambia, Kornelio!


Akaanguka chini, akasikia sauti ikimwambia, Sauli, Sauli, mbona wanitesa?


Na kwa vitu vilivyo bora vya nchi, na kujaa kwake, Na uradhi wake aliyekaa ndani ya kile kichaka; Na ije baraka juu ya kichwa chake Yusufu, Juu ya utosi wa kichwa chake aliyetengwa na nduguze.


BWANA akaja, akasimama, akaita vile vile kama kwanza, Samweli! Samweli! Ndipo Samweli akasema, Nena, BWANA; kwa kuwa mtumishi wako anasikia.


basi, wakati huo BWANA akamwita Samweli; naye akasema, Mimi hapa.


BWANA akaita mara ya pili, Samweli! Samweli! Akaondoka akamwendea Eli, akasema, Mimi hapa; kwa maana uliniita. Akajibu, Sikukuita, mwanangu; kalale tena.


BWANA akamwita Samweli mara ya tatu. Naye akaondoka akamwendea Eli, akasema, Mimi hapa; kwa maana uliniita. Ndipo Eli akatambua ya kuwa BWANA ndiye aliyemwita yule mtoto.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo