Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Kutoka 29:26 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

26 Kisha twaa kidari cha huyo kondoo wa kuwekwa kwake Haruni kwa kazi takatifu, na kukitikisatikisa kiwe sadaka ya kutikiswa mbele za BWANA; nacho kitakuwa ni sehemu yako.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

26 “Kisha utachukua kidari cha huyo kondoo wa kumweka wakfu Aroni, na kufanya ishara ya kunitolea mimi Mwenyezi-Mungu. Nacho kitakuwa sehemu yako.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

26 “Kisha utachukua kidari cha huyo kondoo wa kumweka wakfu Aroni, na kufanya ishara ya kunitolea mimi Mwenyezi-Mungu. Nacho kitakuwa sehemu yako.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

26 “Kisha utachukua kidari cha huyo kondoo wa kumweka wakfu Aroni, na kufanya ishara ya kunitolea mimi Mwenyezi-Mungu. Nacho kitakuwa sehemu yako.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

26 Baada ya kuchukua kidari cha huyo kondoo dume wa kuwekwa wakfu kwa Haruni, kiinue mbele za Mwenyezi Mungu kuwa sadaka ya kuinuliwa, nayo itakuwa fungu lako.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

26 Baada ya kuchukua kidari cha huyo kondoo dume wa kuwekwa wakfu kwa Haruni, kiinue mbele za bwana kuwa sadaka ya kuinuliwa, nayo itakuwa fungu lako.

Tazama sura Nakili




Kutoka 29:26
8 Marejeleo ya Msalaba  

Musa na Haruni walikuwa makuhani wake, Na Samweli pia ni miongoni mwa walioliitia jina lake, Walimlilia BWANA naye akawaitikia;


Nawe kitakase kile kidari cha ile sadaka ya kutikiswa, na lile paja la sadaka ya kuinuliwa, lililotikiswa, na lililoinuliwa juu, vya yule kondoo wa kuwekwa kwa kazi takatifu, huyo aliyekuwa kwa ajili ya Haruni, na huyo aliyekuwa kwa ajili ya wanawe;


kisha kuhani atamshika mmoja kati ya hao wana-kondoo wa kiume, na kumsongeza awe sadaka ya hatia, pamoja na hiyo logi ya mafuta, kisha atavitikisa kuwa ni sadaka ya kutikiswa mbele za BWANA;


mikono yake mwenyewe itamletea hizo sadaka za kusongezwa kwa moto; mafuta yake pamoja na kidari atavileta, ili kwamba hicho kidari kitikiswe kuwa sadaka ya kutikiswa mbele ya BWANA.


Kuhani atayateketeza hayo mafuta juu ya madhabahu; lakini hicho kidari kitakuwa cha Haruni na wanawe.


Kwa maana, hicho kidari cha kutikiswa, na huo mguu wa kuinuliwa, nimevitwaa kwa wana wa Israeli, katika dhabihu zao za sadaka za amani, nami nimempa Haruni kuhani na wanawe, kuwa haki yao ya milele kutoka kwa wana wa Israeli.


Kisha Musa akakitwaa kile kidari, akakitikisa huku na huko, kiwe sadaka ya kutikiswa mbele za BWANA; ni sehemu ya Musa katika huyo kondoo dume wa kuwaweka wakfu; kama BWANA alivyomwagiza Musa.


na vile vidari, na mguu wa nyuma wa upande wa kulia, Haruni akavitikisa huku na huku viwe sadaka ya kutikiswa mbele ya BWANA; kama Musa alivyoagiza.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo