Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Kutoka 29:20 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

20 Kisha utamchinja kondoo, na kuitwaa damu yake, na kuitia katika ncha ya sikio la Haruni la upande wa kulia, na katika ncha za masikio ya kulia ya wanawe, na katika vyanda vya gumba vya mikono yao ya kulia, na katika vidole vikuu vya miguu yao ya kulia, na kuinyunyiza hiyo damu katika madhabahu kuizunguka kandokando.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

20 Nawe utamchinja na kuchukua kiasi cha damu na kumpaka Aroni na wanawe kwenye ncha za masikio yao ya kulia na vidole gumba vya mikono yao ya kulia, na vidole gumba vya miguu yao ya kulia. Damu inayobaki utairashia madhabahu pande zake zote.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

20 Nawe utamchinja na kuchukua kiasi cha damu na kumpaka Aroni na wanawe kwenye ncha za masikio yao ya kulia na vidole gumba vya mikono yao ya kulia, na vidole gumba vya miguu yao ya kulia. Damu inayobaki utairashia madhabahu pande zake zote.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

20 Nawe utamchinja na kuchukua kiasi cha damu na kumpaka Aroni na wanawe kwenye ncha za masikio yao ya kulia na vidole gumba vya mikono yao ya kulia, na vidole gumba vya miguu yao ya kulia. Damu inayobaki utairashia madhabahu pande zake zote.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

20 Mchinje, uchukue sehemu ya damu yake na kuipaka kwenye masikio ya Haruni na wanawe, kwenye vidole gumba vya mikono yao ya kuume, pia kwenye vidole gumba vya miguu yao ya kuume. Kisha nyunyiza hiyo damu pande zote za madhabahu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

20 Mchinje, uchukue sehemu ya damu yake na kuipaka kwenye masikio ya Haruni na wanawe, kwenye vidole gumba vya mikono yao ya kuume, pia kwenye vidole gumba vya miguu yao ya kuume. Kisha nyunyiza hiyo damu pande zote za madhabahu.

Tazama sura Nakili




Kutoka 29:20
19 Marejeleo ya Msalaba  

Kisha mtwae huyo kondoo wa pili; na Haruni na wanawe wataweka mikono yao juu ya kichwa chake huyo kondoo.


Kisha twaa katika hiyo damu iliyo juu ya madhabahu, na katika hayo mafuta ya kutiwa, na kumnyunyizia Haruni, juu ya mavazi yake, na wanawe, na mavazi yao pia, pamoja naye; naye atatakaswa, na mavazi yake, na wanawe, na mavazi ya wanawe, pamoja naye.


Bwana MUNGU amenizibua sikio langu, wala sikuwa mkaidi, wala sikurudi nyuma.


ndivyo atakavyowastusha mataifa mengi; wafalme watamfumbia vinywa vyao; maana mambo wasiyoambiwa watayaona; na mambo wasiyoyasikia watayafahamu.


kisha huyo kuhani atatwaa baadhi ya hiyo damu ya sadaka ya hatia, naye kuhani ataitia katika ncha ya sikio la kulia la huyo atakayetakaswa, na katika kidole cha gumba cha mkono wake wa kulia, na katika kidole kikuu cha mguu wake wa kulia;


kisha kuhani atatia kidole cha mkono wa kulia katika hayo mafuta, yaliyo katika mkono wake wa kushoto, naye atayanyunyiza hayo mafuta kwa kidole chake mara saba mbele za BWANA;


na katika yale mafuta yaliyobaki mkononi mwake kuhani atayatia katika ncha ya sikio la kulia la huyo atakayetakaswa, na katika kidole cha gumba cha mkono wake wa kulia, na katika kidole kikuu cha mguu wake wa kulia, juu ya damu ya sadaka ya hatia;


kisha atamchinja mwana-kondoo wa sadaka ya hatia, na kuhani atatwaa katika damu ya sadaka ya hatia, na kuitia katika ncha ya sikio la kulia la huyo atakayetakaswa, na katika kidole cha gumba cha mkono wake wa kulia, na katika kidole kikuu cha mguu wake wa kulia;


kisha kuhani atatia mengine katika hayo mafuta yaliyo mkononi mwake katika ncha ya sikio la kulia la huyo atakayetakaswa, na katika kidole cha gumba cha mkono wake wa kulia, na katika kidole kikuu cha mguu wake wa kulia, juu ya mahali pale penye damu ya sadaka ya hatia;


kisha atamnyunyizia huyo atakayetakaswa na ukoma mara saba, naye atasema kwamba ni safi, kisha atamwacha yule ndege aliye hai aende zake nyikani.


Tena atanyunyiza baadhi ya damu juu ya madhabahu kwa kidole chake mara saba, na kuitakasa, ili machafu yote ya wana wa Israeli yaitoke.


Kisha akamchinja; na Musa akatwaa baadhi ya damu yake, na kuitia katika ncha ya sikio la kulia la Haruni, na katika kidole cha gumba cha mkono wake wa kulia, na katika kidole cha gumba cha guu lake la kulia.


Kisha akawaleta wana wa Haruni, na Musa akaitia hiyo damu katika ncha za masikio ya upande wa kulia, na katika vidole vya gumba vya mikono yao ya kulia, na katika vidole vya gumba vya maguu yao ya kulia; kisha Musa akainyunyiza hiyo damu katika madhabahu pande zote.


Akamtenga na mkutano faraghani, akatia vidole vyake masikioni mwake, akatema mate, akamgusa ulimi,


na tukaribie wenye moyo wa kweli, kwa utimilifu wa imani, hali tumenyunyiziwa mioyo tuache dhamiri mbaya, tumeoshwa miili kwa maji safi.


na Yesu mjumbe wa agano jipya, na damu ya kunyunyizwa, inenayo mema kuliko ile ya Habili.


kama vile Mungu Baba alivyotangulia kuwajua katika kutakaswa na Roho, hata mkapata kutii na kunyunyiziwa damu ya Yesu Kristo. Neema na amani na ziongezwe kwenu.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo