Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Kutoka 28:9 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

9 Nawe utatwaa vito viwili vya shohamu rangi ya chanikiwiti, nawe utachora juu yake majina ya wana wa Israeli;

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

9 “Kisha utachukua mawe mawili ya sardoniki ambayo utachora juu yake majina ya wana wa Israeli.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

9 “Kisha utachukua mawe mawili ya sardoniki ambayo utachora juu yake majina ya wana wa Israeli.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

9 “Kisha utachukua mawe mawili ya sardoniki ambayo utachora juu yake majina ya wana wa Israeli.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

9 “Chukua vito viwili vya shohamu, na uchore juu yake majina ya wana wa Israeli

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

9 “Chukua vito viwili vya shohamu, na uchore juu yake majina ya wana wa Israeli

Tazama sura Nakili




Kutoka 28:9
16 Marejeleo ya Msalaba  

na dhahabu ya nchi ile ni njema; huko kuna bedola, na vito shoham.


Basi kwa uwezo wangu wote nimeiwekea akiba nyumba ya Mungu wangu, dhahabu kwa vitu vya dhahabu, na fedha kwa vitu vya fedha, na shaba kwa vitu vya shaba, na chuma kwa vitu vya chuma, na miti kwa vitu vya miti; vito vya shohamu, na vya kujazia, vito vya njumu, na vya rangi mbalimbali, na mawe ya thamani ya kila namna, na marumaru tele.


Unitumie mtu stadi wa kuchonga dhahabu, fedha, shaba na chuma, na wa nguo za urujuani, nyekundu na samawati, ajuaye kutia nakshi, awe mmoja wa mastadi walioko pamoja nami Yuda na Yerusalemu ambao aliwaweka baba yangu Daudi.


Haiwezi kutiwa thamani kwa dhahabu ya Ofiri, Wala kwa shohamu ya thamani nyingi, wala kwa yakuti samawi.


na vito vya shohamu, na vito vingine vya kutiwa kwa ile naivera, na kwa kile kifuko cha kifuani.


majina yao sita katika kito kimoja, na majina sita yaliyosalia katika kile kito cha pili, kwa utaratibu wa kuzaliwa kwao.


na safu ya nne itakuwa ni zabarajadi, shohamu na yaspi; vito hivyo vitakazwa ndani ya dhahabu kwa kujaa mahali pake.


Nawe fanya bamba la dhahabu safi na kuchora juu yake, mfano wa michoro ya mihuri, MTAKATIFU KWA BWANA.


Na mshipi stadi ulio juu yake, ili kuifunga mahali pake; utakuwa wa kazi kama ile ya naivera, ya vitu vile vile ya nyuzi za dhahabu, za buluu, zambarau na nyekundu, na kitani nzuri yenye kusokotwa.


na kukata vito kwa kutiwa mahali, na kuchora miti, na kufanya kazi ya ustadi iwayo yote.


Na safu ya nne ilikuwa ni zabarajadi, na shohamu, na yaspi: vito hivyo vilikuwa vimetiwa katika vijalizo vya dhahabu, kila kimoja mahali pake.


Nao wakavitengeza vile vito vya shohamu, vilivyotiwa katika vijalizo vya dhahabu, vilivyochorwa mfano wa kuchora kwake mhuri, kwa majina ya hao wana wa Israeli.


Nitie kama mhuri moyoni mwako, Kama mhuri juu ya mkono wako; Kwa maana upendo una nguvu kama mauti, Na wivu ni mkali kama ahera. Mwako wake ni mwako wa moto, Na miali yake ni miali ya Yahu.


Tazama, nimekuchora katika vitanga vya mikono yangu; kuta zako ziko mbele zangu daima.


Ulikuwa ndani ya Adeni, bustani ya Mungu; kila jiwe la thamani lilikuwa kifuniko chako, akiki, na yakuti manjano, na almasi, na zabarajadi, na shohamu, na yaspi, na yakuti samawi, na zumaridi, na baharamani, na dhahabu; kazi ya matari yako na filimbi zako ilikuwa ndani yako; katika siku ya kuumbwa kwako zilitengenezwa tayari.


Na BWANA, Mungu wao, atawaokoa siku hiyo, Kama kundi la watu wake; Kwa maana watakuwa kama vito vya taji, Vikimetameta juu ya nchi yake.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo