Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Kutoka 28:37 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

37 Nawe ulitie hilo bamba katika ukanda wa rangi ya buluu, nalo litakuwa katika kile kilemba; litakuwa upande wa mbele wa kile kilemba.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

37 Kibati hicho utakifunga mbele ya kilemba kwa ukanda wa buluu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

37 Kibati hicho utakifunga mbele ya kilemba kwa ukanda wa buluu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

37 Kibati hicho utakifunga mbele ya kilemba kwa ukanda wa buluu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

37 Lifunge hilo bamba kwa kamba ya buluu kwenye kilemba, nalo ni lazima liwe mbele ya kilemba.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

37 Lifunge hilo bamba kwa kamba ya buluu kwenye kilemba, nalo ni lazima liwe mbele ya kilemba.

Tazama sura Nakili




Kutoka 28:37
10 Marejeleo ya Msalaba  

Nao watakikaza kile kileso kwa zile pete zake kwenye pete za naivera kwa ukanda wa rangi ya samawati, ili kwamba kikae pale juu ya ule mshipi wa naivera uliosukwa kwa ustadi, ili kwamba kifuko cha kifuani kisiachane na naivera.


Nawe fanya hiyo joho la naivera ya rangi ya buluu yote.


Nawe fanya bamba la dhahabu safi na kuchora juu yake, mfano wa michoro ya mihuri, MTAKATIFU KWA BWANA.


Nalo litakuwa katika kipaji cha uso cha Haruni, na Haruni atauchukua uovu wa vile vitu vitakatifu, watakavyovitakasa hao wana wa Israeli katika vipawa vyao vyote vitakatifu, nalo litakuwa katika kipaji chake cha uso sikuzote, ili vipate kukubaliwa mbele za BWANA.


Na mavazi watakayoyafanya ni haya; kifuko cha kifuani, na naivera, na joho, na kanzu ya kazi ya urembo; na kilemba, na mshipi; nao watawafanyia Haruni nduguyo, na wanawe, mavazi matakatifu ili anitumikie katika kazi ya ukuhani.


nawe mvike kile kilemba kichwani, na lile taji takatifu utalitia katika kile kilemba.


Akamvika na kile kilemba kichwani mwake; na juu ya kilemba, upande wa mbele, akakitia kile kipande cha dhahabu, hilo taji takatifu; kama BWANA alivyomwagiza Musa.


Nikasema, Na wampige kilemba kizuri kichwani pake. Basi, wakampiga kilemba kizuri kichwani pake, wakamvika mavazi; naye malaika wa BWANA akasimama karibu.


Nena na wana wa Israeli, na kuwaagiza ya kwamba wajifanyie vishada katika ncha za nguo zao, katika vizazi vyao, tena ya kwamba watie katika kila kishada cha kila ncha nyuzi za rangi ya buluu;


Tufuate:

Matangazo


Matangazo