Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -

Kutoka 28:32 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

32 Nayo itakuwa na tundu katikati yake kwa kupitisha kichwa; itakuwa na utepe wa kazi ya kusokotwa kuzunguka hilo tundu lake, mfano wa tundu lililo katika kanzu ya chuma, ili lisipasuke.

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

32 Itakuwa na nafasi ya kupitishia kichwa katikati, na nafasi hiyo itazungushiwa utepe uliofumwa ili isichanike.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

32 Itakuwa na nafasi ya kupitishia kichwa katikati, na nafasi hiyo itazungushiwa utepe uliofumwa ili isichanike.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

32 Itakuwa na nafasi ya kupitishia kichwa katikati, na nafasi hiyo itazungushiwa utepe uliofumwa ili isichanike.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

32 na katikati uweke nafasi ya kuingizia kichwa. Kutakuwa na utepe uliofumwa, unaofanana na ukosi kuizunguka nafasi hiyo, ili isichanike.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

32 na katikati uweke nafasi ya kuingizia kichwa. Kutakuwa na utepe uliofumwa, unaofanana na ukosi kuizunguka nafasi hiyo, ili isichanike.

Tazama sura Nakili

Kutoka 28:32
9 Marejeleo ya Msalaba  

Uzia akawapatia jeshi lote ngao na mikuki, na chapeo, na deraya za madini, na nyuta, na mawe ya kupiga kwa teo.

Ikawa tokea wakati huo, nusu ya watumishi wangu walitumika katika kazi hiyo, na nusu yao wakaishika mikuki, na ngao, na pinde, na darii; na viongozi walikuwa nyuma ya nyumba yote ya Yuda.

Mtu akimpiga kwa upanga, haumwingii; Wala fumo, wala mshale, wala mkuki wenye ncha.

Nawe fanya hiyo joho la naivera ya rangi ya buluu yote.

Nawe katika pindo zake utatia makomamanga ya rangi ya buluu, zambarau na nyekundu, kuzunguka pindo zake kotekote; na njuga za dhahabu kati ya hayo makomamanga pande zote;

na hilo tundu lililokuwa katikati yake, mfano wa tundu lililo katika kanzu ya chuma, na utepe wake kulizunguka hilo tundu, ili lisipasuke.

na hicho kilemba cha nguo ya kitani nzuri, na zile kofia nzuri za kitani, na hizo suruali za nguo ya kitani nzuri iliyosokotwa,

Tufuate:

Matangazo

Matangazo