Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Kutoka 28:30 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

30 Nawe utie hizo Urimu na Thumimu katika kile kifuko cha kifuani cha hukumu; nazo zitakuwa juu ya moyo wa Haruni, hapo atakapoingia ndani mbele ya BWANA; na Haruni atachukua hukumu ya hao wana wa Israeli juu ya moyo wake mbele ya BWANA daima.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

30 Kwenye kifuko hicho utatia mawe ya kauli yaninginie kifuani mwa Aroni kila anapokuja mbele yangu. Nyakati hizo ni lazima kila mara kuvaa kifuko hicho, ili aweze kutambua matakwa yangu kuhusu Waisraeli.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

30 Kwenye kifuko hicho utatia mawe ya kauli yaninginie kifuani mwa Aroni kila anapokuja mbele yangu. Nyakati hizo ni lazima kila mara kuvaa kifuko hicho, ili aweze kutambua matakwa yangu kuhusu Waisraeli.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

30 Kwenye kifuko hicho utatia mawe ya kauli yaning'inie kifuani mwa Aroni kila anapokuja mbele yangu. Nyakati hizo ni lazima kila mara kuvaa kifuko hicho, ili aweze kutambua matakwa yangu kuhusu Waisraeli.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

30 Pia weka Urimu na Thumimu ndani ya kifuko cha kifuani, yawe juu ya moyo wa Haruni kila mara aingiapo mbele za Mwenyezi Mungu. Kwa hiyo siku zote Haruni atakuwa na uwezo kufanya maamuzi kwa ajili ya Waisraeli mbele za Mwenyezi Mungu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

30 Pia weka Urimu na Thumimu ndani ya kifuko cha kifuani, yawe juu ya moyo wa Haruni kila mara aingiapo mbele za bwana. Kwa hiyo siku zote Haruni atakuwa na uwezo kufanya maamuzi kwa ajili ya wana wa Israeli mbele za bwana.

Tazama sura Nakili




Kutoka 28:30
22 Marejeleo ya Msalaba  

Na huyo Tirshatha akawaambia kwamba wasile katika vitu vitakatifu sana, hata atakaposimama kuhani mwenye Urimu na Thumimu.


Na huyo Tirshatha akawaambia kwamba wasile katika vile vitu vitakatifu sana, hata atakaposimama kuhani mwenye Urimu na Thumimu.


Na Haruni atayachukua majina ya wana wa Israeli katika kile kifuko cha kifuani cha hukumu juu ya moyo wake, hapo atakapoingia ndani ya mahali patakatifu, kuwa ukumbusho mbele ya BWANA daima.


Kisha akamtia kile kifuko cha kifuani; akatia hizo Urimu na Thumimu katika hicho kifuko cha kifuani.


Naam, yeye atalijenga hekalu la BWANA; naye atakuwa na heshima ya kifalme; na ataketi na kutawala; na kutakuwa na kuhani katika kiti chake cha enzi; na maelewano yenye amani yatakuwa kati ya hao wawili.


Naye atasimama mbele ya Eleazari kuhani, naye atamwulizia kwa hukumu ya ile Urimu mbele za BWANA; kwa neno lake watatoka, na kwa neno lake wataingia; yeye na wana wa Israeli wote pamoja naye, mkutano wote pia.


Nami nitakuwa radhi kutumia na kutumiwa kwa ajili yenu. Je! Kadiri nizidivyo kuwapenda sana, ninapungukiwa kupendwa?


Sisemi neno hilo ili niwahukumu ninyi kuwa na hatia; kwa maana nimetangulia kusema, ya kwamba ninyi mmo mioyoni mwetu hata kwa kufa pamoja, na kuishi pamoja.


Akamnena Lawi, Thumimu yako na Urimu yako vina mtakatifu wako, Uliyemjaribu huko Masa; Ukateta naye kwenye maji ya Meriba.


Hivyo ilimpasa kufananishwa na ndugu zake katika mambo yote, apate kuwa kuhani mkuu mwenye rehema, mwaminifu katika mambo ya Mungu, ili afanye kafara ya suluhu kwa dhambi za watu wake.


Kwa kuwa hamna kuhani mkuu asiyeweza kuchukuana nasi katika mambo yetu ya udhaifu; bali yeye alijaribiwa kama sisi katika mambo yote, bila kufanya dhambi.


wala si kwa damu ya mbuzi na ndama, bali kwa damu yake mwenyewe aliingia mara moja tu katika Patakatifu, akiisha kupata ukombozi wa milele.


Kwa sababu Kristo hakuingia katika patakatifu palipofanyika kwa mikono, ndio mfano wa patakatifu halisi; bali aliingia mbinguni hasa, aonekane sasa usoni pa Mungu kwa ajili yetu;


Ikawa baada ya kufa kwake Yoshua, wana wa Israeli wakamwuliza BWANA, wakisema, Ni nani atakayekwea kwanza kwa ajili yetu juu ya Wakanaani, ili kupigana nao?


Basi wana wa Israeli wakainuka, wakakwea kwenda Betheli, nao wakataka shauri kwa Mungu; wakasema, Ni nani atakayekwea kwenda vitani kwanza kwa ajili yetu juu ya wana wa Benyamini? BWANA akawaambia, Yuda atakwea kwanza.


Wana wa Israeli wakakwea juu na kulia mbele za BWANA hadi jioni; wakamwuliza BWANA, wakisema, Je! Niende nikaribie tena kupiga vita juu ya wana wa Benyamini ndugu yangu? BWANA akasema, Haya, kweeni, mwende kupigana naye.


Lakini Sauli alipouliza kwa BWANA, BWANA hakumjibu, wala kwa ndoto, wala kwa Urimu, wala kwa manabii.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo