Kutoka 27:21 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC21 Ndani ya ile hema ya kukutania, nje ya hilo pazia, lililo mbele ya huo ushuhuda, Haruni na wanawe wataitengeza tangu jioni hadi asubuhi mbele ya BWANA; itakuwa ni amri ya milele katika vizazi vyao vyote kwa ajili ya wana wa Israeli. Tazama suraMatoleo zaidiBiblia Habari Njema21 Hiyo itakuwa ndani ya hema la mkutano nje ya pazia hilo mbele ya sanduku la maamuzi na Aroni na wanawe wataitunza mbele yangu tangu jioni mpaka asubuhi. Agizo hili sharti lifuatwe daima na Waisraeli wote, kizazi hata kizazi. Tazama suraBiblia Habari Njema - BHND21 Hiyo itakuwa ndani ya hema la mkutano nje ya pazia hilo mbele ya sanduku la maamuzi na Aroni na wanawe wataitunza mbele yangu tangu jioni mpaka asubuhi. Agizo hili sharti lifuatwe daima na Waisraeli wote, kizazi hata kizazi. Tazama suraBiblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza21 Hiyo itakuwa ndani ya hema la mkutano nje ya pazia hilo mbele ya sanduku la maamuzi na Aroni na wanawe wataitunza mbele yangu tangu jioni mpaka asubuhi. Agizo hili sharti lifuatwe daima na Waisraeli wote, kizazi hata kizazi. Tazama suraNeno: Bibilia Takatifu21 Katika Hema la Kukutania, nje ya pazia lililo mbele ya Sanduku la Ushuhuda, Haruni na wanawe watahakikisha kuwa taa hizo zinawaka kuanzia jioni hadi asubuhi mbele za Mwenyezi Mungu. Hili litakuwa agizo la milele miongoni mwa Waisraeli kwa vizazi vijavyo. Tazama suraNeno: Maandiko Matakatifu21 Katika Hema la Kukutania, nje ya pazia lililo mbele ya Sanduku la Ushuhuda, Haruni na wanawe watahakikisha kuwa taa hizo zinawaka kuanzia jioni mpaka asubuhi mbele za bwana. Hili litakuwa agizo la milele miongoni mwa Waisraeli kwa vizazi vyote vijavyo. Tazama sura |
nao humtolea BWANA kila asubuhi, na kila jioni, sadaka za kuteketezwa na fukizo la manukato; mikate ya wonyesho pia huiweka kwa taratibu yake juu ya meza takatifu, na kinara cha dhahabu chenye taa zake, kuwaka kila jioni; kwa maana sisi tunayatunza maagizo ya BWANA, Mungu wetu; bali ninyi mmemwacha.