Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -

Kutoka 27:10 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

10 na nguzo zake zitakuwa nguzo ishirini, na vitako vyake ishirini, vitako vyake vitakuwa vya shaba; kulabu za zile nguzo na vitanzi vyake vitakuwa vya fedha.

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

10 Vyandarua hivyo vitashikiliwa na nguzo ishirini za shaba zenye vikalio vya shaba. Lakini kulabu za nguzo hizo na vitanzi vyake vitakuwa vya fedha.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

10 Vyandarua hivyo vitashikiliwa na nguzo ishirini za shaba zenye vikalio vya shaba. Lakini kulabu za nguzo hizo na vitanzi vyake vitakuwa vya fedha.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

10 Vyandarua hivyo vitashikiliwa na nguzo ishirini za shaba zenye vikalio vya shaba. Lakini kulabu za nguzo hizo na vitanzi vyake vitakuwa vya fedha.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

10 pamoja na nguzo ishirini na vitako vya shaba ishirini, na kulabu na tepe za fedha juu ya hizo nguzo.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

10 pamoja na nguzo ishirini na vitako vya shaba ishirini, na kulabu na tepe za fedha juu ya hizo nguzo.

Tazama sura Nakili

Kutoka 27:10
7 Marejeleo ya Msalaba  

Ni vivyo hivyo upande wa kaskazini, urefu wake hiyo chandarua utakuwa ni dhiraa mia moja, na nguzo zake ishirini, na vitako vyake ishirini vitakuwa vya shaba; kulabu za zile nguzo na vitanzi vyake vitakuwa vya fedha.

Nawe fanya ua wa maskani; upande wa kusini wa kuelekea kusini kutakuwa na chandarua ya nguo ya kitani nzuri yenye kusokotwa, kwa huo ua, urefu wake upande mmoja utakuwa ni dhiraa mia moja;

na nguzo zake tano pamoja na kulabu zake; naye akavifunika dhahabu vichwa vyake na vifungo vyake; na vitako vyake vitano vilikuwa ya shaba.

nguzo zake zilikuwa ishirini, na vitako vyake vilikuwa ishirini, vilikuwa vya shaba; kulabu za nguzo na vitanzi vyake vilikuwa vya fedha.

na vitako vya ua kuuzunguka pande zote, na vitako vya lango la huo ua, na vigingi vyote vya maskani, na vigingi vyote vya huo ua uliozunguka pande zote.

Na nguzo hizo, urefu wa nguzo moja ulikuwa dhiraa kumi na nane, na uzi wa dhiraa kumi na mbili ungeweza kuizunguka; na unene wake ulikuwa nyanda nne; nayo ilikuwa ya uvungu.

Tufuate:

Matangazo

Matangazo