Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -

Kutoka 26:33 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

33 Nawe tungika lile pazia chini ya vile vifungo, nawe lete lile sanduku la ushuhuda na kulitia humo nyuma ya pazia; na lile pazia litawagawanyia kati ya patakatifu, na mahali patakatifu sana.

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

33 Utalitundika pazia hilo kwenye vifungo, kisha ulilete lile sanduku la ushuhuda humo ndani kukiwa na vibao viwili vya mawe, nyuma ya pazia hilo. Pazia hilo litatenga mahali patakatifu na mahali patakatifu sana.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

33 Utalitundika pazia hilo kwenye vifungo, kisha ulilete lile sanduku la ushuhuda humo ndani kukiwa na vibao viwili vya mawe, nyuma ya pazia hilo. Pazia hilo litatenga mahali patakatifu na mahali patakatifu sana.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

33 Utalitundika pazia hilo kwenye vifungo, kisha ulilete lile sanduku la ushuhuda humo ndani kukiwa na vibao viwili vya mawe, nyuma ya pazia hilo. Pazia hilo litatenga mahali patakatifu na mahali patakatifu sana.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

33 Ning’iniza pazia hilo kwenye vifungo, kisha weka Sanduku la Ushuhuda nyuma ya pazia. Pazia litatenganisha Mahali Patakatifu kutoka Patakatifu pa Patakatifu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

33 Ning’iniza pazia hilo kwenye vifungo, kisha weka Sanduku la Ushuhuda nyuma ya pazia. Pazia litatenganisha Mahali Patakatifu kutoka Patakatifu pa Patakatifu.

Tazama sura Nakili

Kutoka 26:33
16 Marejeleo ya Msalaba  

Akajenga mikono ishirini pande za nyuma za nyumba toka chini hata juu kwa mbao za mwerezi; naam, ndani akaijengea chumba cha ndani, yaani, patakatifu pa patakatifu.

Ikawa, makuhani walipotoka katika patakatifu, nyumba ya BWANA ikajaa wingu;

Makuhani wakalileta sanduku la Agano la BWANA hadi mahali pake, katika chumba cha ndani cha ile nyumba, patakatifu pa patakatifu, naam, chini ya mbawa za makerubi.

Akaifanya nyumba ya patakatifu pa patakatifu; urefu wake sawa na upana wa nyumba, ulikuwa dhiraa ishirini, na upana wake dhiraa ishirini; akaifunikiza kwa dhahabu safi, ya talanta mia sita.

Kisha tia ndani ya sanduku huo ushuhuda nitakaokupa.

kisha litungike katika nguzo nne za mti wa mshita zilizofunikwa dhahabu, vifungo vyake vitakuwa vya dhahabu, katika vitako vya fedha vinne.

na nguzo zake zitakuwa nguzo ishirini, na vitako vyake ishirini, vitako vyake vitakuwa vya shaba; kulabu za zile nguzo na vitanzi vyake vitakuwa vya fedha.

Ndani ya ile hema ya kukutania, nje ya hilo pazia, lililo mbele ya huo ushuhuda, Haruni na wanawe wataitengeza tangu jioni hadi asubuhi mbele ya BWANA; itakuwa ni amri ya milele katika vizazi vyao vyote kwa ajili ya wana wa Israeli.

Naye akafanya kwa ajili yake nguzo nne za mti wa mshita, akazifunika dhahabu; na kulabu zake zilikuwa za dhahabu; naye akasubu kwa ajili yake vitako vinne vya fedha.

kisha akalileta sanduku akalitia ndani ya maskani, naye akalitundika pazia la sitara, akalisitiri sanduku la ushuhuda; kama BWANA alivyomwamuru Musa.

Nawe utatia ndani yake sanduku la ushuhuda, nawe utalisitiri hilo sanduku kwa pazia.

Akaupima urefu wake; dhiraa ishirini, na upana wake, dhiraa ishirini, mbele ya hekalu; akaniambia, Hapa ndipo mahali patakatifu kuliko kila mahali.

BWANA akamwambia Musa, Mwambie Haruni ndugu yako, kwamba asiingie wakati wowote katika mahali patakatifu ndani ya pazia, mbele ya kiti cha rehema, kilicho juu ya sanduku, asije akafa; maana, mimi nitaonekana katika lile wingu juu ya kiti cha rehema.

Tufuate:

Matangazo

Matangazo