Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -

Kutoka 26:32 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

32 kisha litungike katika nguzo nne za mti wa mshita zilizofunikwa dhahabu, vifungo vyake vitakuwa vya dhahabu, katika vitako vya fedha vinne.

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

32 Utalitundika pazia kwenye nguzo nne za mjohoro zilizopakwa dhahabu, zenye kulabu za dhahabu na vikalio vinne vya fedha.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

32 Utalitundika pazia kwenye nguzo nne za mjohoro zilizopakwa dhahabu, zenye kulabu za dhahabu na vikalio vinne vya fedha.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

32 Utalitundika pazia kwenye nguzo nne za mjohoro zilizopakwa dhahabu, zenye kulabu za dhahabu na vikalio vinne vya fedha.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

32 Litundike kwa kulabu za dhahabu kwenye nguzo nne za mti wa mshita ambazo zimefunikwa kwa dhahabu, zikiwa zimesimamishwa kwenye vitako vinne vya fedha.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

32 Litundike kwa kulabu za dhahabu kwenye nguzo nne za mti wa mshita ambazo zimefunikwa kwa dhahabu, zikiwa zimesimamishwa kwenye vitako vinne vya fedha.

Tazama sura Nakili

Kutoka 26:32
6 Marejeleo ya Msalaba  

Palikuwa na mapazia ya bafta, nyeupe na samawati, yamefungiwa kamba za kitani safi za rangi ya zambarau kwa pete za fedha na nguzo za marumaru; pia na vitanda vilikuwa vya dhahabu na fedha juu ya sakafu yenye nakshi ya vito vyekundu, marumaru, lulu za manjano na nyeusi na mawe ya thamani.

na ngozi za kondoo dume zilizotiwa rangi nyekundu, na ngozi za pomboo, na miti ya mjohoro,

Nawe fanya pazia la nyuzi za rangi ya buluu, zambarau na nyekundu, na nguo za kitani nzuri zenye kusokotwa, litafumwa na kutiwa makerubi, kazi ya fundi stadi;

Nawe tungika lile pazia chini ya vile vifungo, nawe lete lile sanduku la ushuhuda na kulitia humo nyuma ya pazia; na lile pazia litawagawanyia kati ya patakatifu, na mahali patakatifu sana.

Nawe fanya nguzo tano za mti wa mshita kwa kile kisitiri, na kuzifunika dhahabu; kulabu zake zitakuwa za dhahabu; nawe utasubu vitako vya shaba vitano kwa ajili yake.

na nguzo zake tano pamoja na kulabu zake; naye akavifunika dhahabu vichwa vyake na vifungo vyake; na vitako vyake vitano vilikuwa ya shaba.

Tufuate:

Matangazo

Matangazo