Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Kutoka 25:40 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

40 Nawe angalia ya kwamba uvifanye kama mfano wake, uliooneshwa mlimani.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

40 Hakikisha kwamba umevitengeneza kwa mfano uliooneshwa kule mlimani.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

40 Hakikisha kwamba umevitengeneza kwa mfano uliooneshwa kule mlimani.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

40 Hakikisha kwamba umevitengeneza kwa mfano uliooneshwa kule mlimani.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

40 Hakikisha kuwa umevitengeneza sawasawa na ule mfano uliooneshwa kule mlimani.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

40 Hakikisha kuwa umevitengeneza sawasawa na ule mfano ulioonyeshwa kule mlimani.

Tazama sura Nakili




Kutoka 25:40
15 Marejeleo ya Msalaba  

Ndipo Daudi akampa Sulemani mwanawe mfano wa ukumbi wa hekalu, na nyumba zake, na hazina zake, na ghorofa zake, na vyumba vyake vya ndani, na mahali pa kiti cha rehema;


Hayo yote, akasema Daudi, yamenielea kwa maandiko kutoka kwa mkono wa BWANA, naam, kazi zote za mfano huu.


Alivitengeneza vinara vya taa kumi vya dhahabu, kama vilivyoagiziwa; akavitia hekaluni, vitano upande wa kulia, na vitano upande wa kushoto.


Kitafanywa cha talanta moja ya dhahabu safi, pamoja na vyombo hivi vyote.


Sawasawa na haya yote nikuoneshayo, mfano wa maskani, na mfano wa samani zake zote, ndivyo mtakavyovifanya.


Nawe utaisimamisha hiyo maskani sawasawa na mfano wake uliooneshwa mlimani.


Uifanye ya mbao, yenye mvungu ndani yake; kama ulivyooneshwa mlimani, ndivyo watakavyoifanya.


na mafuta ya kutiwa, na uvumba wa manukato mazuri, kwa ajili ya mahali patakatifu; sawasawa na yote niliyokuagiza ndivyo watakavyofanya wao.


Basi Musa akawaita Bezaleli na Oholiabu, na kila mtu aliyekuwa na moyo wa akili, ambaye BWANA alimtia moyoni mwake hekima, kila mtu ambaye moyo wake ulimhimiza ili aende kuifanya kazi hiyo;


Na hii ndiyo kazi ya hicho kinara cha taa, ilikuwa ni kazi ya ufuzi wa dhahabu; tangu kitako chake hata maua yake kilikuwa ni kazi ya ufuzi; vile vile kama ule mfano BWANA aliokuwa amemwonesha Musa, ndivyo alivyokifanya kinara.


Ile hema ya ushahidi ilikuwa pamoja na baba zetu jangwani, kama alivyoagiza yeye aliyesema na Musa, ya kwamba aifanye kulingana na mfano ule aliouona;


watumikiao mfano na kivuli cha mambo ya mbinguni, kama Musa alivyoagizwa na Mungu, alipokuwa tayari kuifanya ile hema; maana asema, Angalia ukavifanye vitu vyote kwa mfano ule uliooneshwa katika mlima.


Kwa hiyo tulisema, Itakuwa, hapo watakapotuambia neno kama hilo, au kuwaambia watu wa vizazi vyetu katika siku zijazo neno kama hilo, ndipo sisi tutawaambia, Angalieni huu mfano wa madhabahu ya BWANA, walioufanya baba zetu, si kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa, wala kwa ajili ya dhabihu; lakini ni ushahidi kati yetu nanyi.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo