Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Kutoka 25:10 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

10 Nao na wafanye sanduku la mti wa mjohoro; urefu wake na uwe dhiraa mbili na nusu, na upana wake dhiraa moja na nusu, na kwenda juu kwake dhiraa moja na nusu.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

10 “Waisraeli watengeneze sanduku la mbao za mjohoro, lenye urefu wa sentimita 110, upana sentimita 66, na kimo sentimita 66.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

10 “Waisraeli watengeneze sanduku la mbao za mjohoro, lenye urefu wa sentimita 110, upana sentimita 66, na kimo sentimita 66.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

10 “Waisraeli watengeneze sanduku la mbao za mjohoro, lenye urefu wa sentimita 110, upana sentimita 66, na kimo sentimita 66.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

10 “Nao watatengeneza Sanduku la mbao za mshita, lenye urefu wa dhiraa mbili na nusu, upana wa dhiraa moja na nusu, na kimo cha dhiraa moja na nusu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

10 “Nao watatengeneza Sanduku la mbao za mshita, lenye urefu wa dhiraa mbili na nusu, upana wa dhiraa moja na nusu, na kimo cha dhiraa moja na nusu.

Tazama sura Nakili




Kutoka 25:10
11 Marejeleo ya Msalaba  

Sulemani akamleta binti Farao kutoka mji wa Daudi mpaka nyumba aliyomjengea; kwa kuwa alisema, Mke wangu hatakaa nyumbani mwa Daudi mfalme wa Israeli, kwa kuwa ni patakatifu, mahali palipofika sanduku la BWANA.


yaani, hema ya kukutania na sanduku la ushuhuda, na kiti cha rehema kilicho juu yake, na vyombo vyote vya Hema;


hilo sanduku, miti yake, hicho kiti cha rehema na lile pazia la sitara;


Basi ndivyo ilivyomalizwa kazi yote ya maskani ya hema ya kukutania; na wana wa Israeli walifanya kama yote BWANA aliyomwagiza Musa, ndivyo walivyofanya.


Na vitu watakavyovitunza ni hilo sanduku, na meza, na kinara cha taa, na madhabahu, na vile vyombo vya mahali patakatifu wavitumiavyo katika huduma yao, na pazia, na utumishi wake wote.


hapo watakapoanza safari, Haruni ataingia ndani, na wanawe, nao watalishusha pazia la sitara, na kulifunika sanduku la ushahidi kwa hilo pazia;


kisha ataweka juu yake ngozi laini ya mnyama za kulifunikia, na kutandika juu yake nguo ya rangi ya samawati tupu, kisha watatia hiyo miti yake.


yenye chetezo cha dhahabu, na sanduku la Agano lililofunikwa kwa dhahabu pande zote, mlimokuwa na kopo la dhahabu lenye ile mana, na ile fimbo ya Haruni iliyochipuka, na vile vibao vya agano;


Kisha hekalu la Mungu lililoko mbinguni likafunguliwa, na sanduku la Agano lake likaonekana ndani ya hekalu lake. Kukawa na umeme, na sauti, na radi, na tetemeko la nchi, na mvua kubwa ya mawe.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo