Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Kutoka 24:3 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

3 Musa akaenda akawaambia watu maneno yote ya BWANA, na hukumu zake zote; watu wote wakajibu kwa sauti moja, wakasema, Maneno yote aliyoyanena BWANA tutayatenda.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

3 Basi, Mose akaenda na kuwaambia watu wote maneno na maagizo yote Mwenyezi-Mungu aliyomwambia. Watu wote wakajibu kwa sauti moja, “Mambo yote aliyoyasema Mwenyezi-Mungu, tutayafanya.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

3 Basi, Mose akaenda na kuwaambia watu wote maneno na maagizo yote Mwenyezi-Mungu aliyomwambia. Watu wote wakajibu kwa sauti moja, “Mambo yote aliyoyasema Mwenyezi-Mungu, tutayafanya.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

3 Basi, Mose akaenda na kuwaambia watu wote maneno na maagizo yote Mwenyezi-Mungu aliyomwambia. Watu wote wakajibu kwa sauti moja, “Mambo yote aliyoyasema Mwenyezi-Mungu, tutayafanya.”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

3 Musa alipoenda na kuwaambia watu maneno yote na sheria zote za Mwenyezi Mungu, wakaitikia kwa sauti moja, “Kila kitu alichosema Mwenyezi Mungu tutakifanya.”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

3 Musa alipokwenda na kuwaambia watu maneno yote na sheria zote za bwana, wakaitikia kwa sauti moja, “Kila kitu alichosema bwana tutakifanya.”

Tazama sura Nakili




Kutoka 24:3
23 Marejeleo ya Msalaba  

Wakamwapia BWANA kwa sauti kuu, na kwa kelele, na kwa parapanda, na kwa baragumu.


Na Yuda wote wakakifurahia kile kiapo; kwani wameapa kwa moyo wao wote, na kumtafuta kwa mapenzi yao pia; naye ameonekana kwao; naye BWANA akawastarehesha pande zote.


Nikusanyieni wacha Mungu wangu Waliofanya agano nami kwa dhabihu.


Watu wote wakaitika pamoja wakisema, Hayo yote aliyoyasema BWANA tutayatenda. Naye Musa akamwambia BWANA maneno ya hao watu.


na Musa peke yake ndiye atakayekaribia karibu na BWANA; lakini hao hawatakaribia karibu; wala hao watu hawatakwea pamoja naye.


Kisha akakitwaa Kitabu cha Agano akakisoma masikioni mwa watu; wakasema, Hayo yote aliyoyanena BWANA tutayatenda, nasi tutatii.


Niliyowaamuru baba zenu, siku ile nilipowatoa katika nchi ya Misri, katika tanuri ya chuma, nikisema, Itiini sauti yangu, mkafanye sawasawa na yote niwaagizayo ninyi; ndivyo mtakavyokuwa watu wangu, nami nitakuwa Mungu wenu;


BWANA, Mungu wa Israeli, asema hivi, Nilifanya agano na baba zenu, siku ile nilipowatoa katika nchi ya Misri, katika nyumba ya utumwa, nikisema,


kama ilivyo ahadi niliyowawekea mlipotoka katika nchi ya Misri; na roho yangu inakaa kati yenu; msiogope.


Je! Sisi sote hatuna Baba mmoja? Mungu aliyetuumba siye mmoja tu? Basi, mbona kila mmoja wetu anamtenda ndugu yake mambo ya hiana, tukilinajisi agano la baba zetu?


Kwa ajili hii mpende BWANA, Mungu wako, na kushika sikuzote mausia yake, na amri zake, na hukumu zake, na maagizo yake.


Na sasa, Ee Israeli, zisikilizeni amri na hukumu ninazowafundisha, ili mzitende; mpate kuishi na kuingia na kuimiliki nchi anayowapa BWANA, Mungu wa baba zenu.


haya ndiyo maagizo, amri na hukumu, Musa alizowaambia wana wa Israeli walipotoka Misri;


Angalieni nimewafundisha amri na hukumu, vile vile kama BWANA, Mungu wangu, alivyoniamuru, ili mzitende katika nchi mwingiayo ili kuimiliki.


Musa akawaita Israeli wote, akawaambia, Enyi Israeli, zisikieni amri na hukumu nisemazo masikioni mwenu leo, mpate kujifunza na kuzizingatia.


Lakini wewe, simama hapa karibu nami, nami nitasema nawe sheria zote, na amri na hukumu, utakazowafunza, wapate kuzifanya katika nchi niwapayo kuimiliki.


Na hii ndiyo sheria, amri na hukumu, alizoziamuru BWANA, Mungu wenu, mfundishwe, mpate kuzitenda katika nchi ile mnayovuka kuimiliki;


Lakini hao watu wakamwambia Yoshua, La! Lakini tutamtumikia BWANA.


Yoshua akawaambia watu, Ninyi mmekuwa mashahidi juu ya nafsi zenu, ya kuwa mmemchagua BWANA, ili kumtumikia yeye. Wakasema, Sisi tu mashahidi.


Ndipo hao watu wakamwambia Yoshua, BWANA, Mungu wetu, ndiye tutakayemtumikia; na sauti yake ndiyo tutakayoitii.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo