Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Kutoka 24:17 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

17 Na kuonekana kwake ule utukufu wa BWANA kulikuwa kama moto uteketezao, juu ya mlima machoni pa wana wa Israeli.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

17 Utukufu wa Mwenyezi-Mungu ulionekana mbele ya macho ya watu wa Israeli kama moto unaowaka juu ya mlima.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

17 Utukufu wa Mwenyezi-Mungu ulionekana mbele ya macho ya watu wa Israeli kama moto unaowaka juu ya mlima.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

17 Utukufu wa Mwenyezi-Mungu ulionekana mbele ya macho ya watu wa Israeli kama moto unaowaka juu ya mlima.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

17 Kwa Waisraeli utukufu wa Mwenyezi Mungu ulionekana kama moto uteketezao juu ya mlima.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

17 Kwa Waisraeli utukufu wa bwana ulionekana kama moto uteketezao juu ya mlima.

Tazama sura Nakili




Kutoka 24:17
14 Marejeleo ya Msalaba  

Toka mwangaza uliokuwa mbele zake Makaa ya moto yakawashwa.


Kukapanda moshi kutoka puani mwake, Moto ukatoka kinywani mwake ukala; Makaa yakawashwa nao.


wawe tayari kwa siku ya tatu; maana siku ya tatu BWANA atashuka katika mlima wa Sinai machoni pa watu hawa wote.


Mlima wa Sinai wote pia ukatoa moshi, kwa sababu BWANA alishuka katika moto; na ule moshi wake ukapanda juu kama moshi wa tanuri, mlima wote ukatetemeka sana.


Malaika wa BWANA akamtokea, katika mwali wa moto uliotoka katikati ya kichaka; akatazama, na kumbe! Kile kichaka kiliwaka moto, nacho kichaka hakikuteketea.


Nikaona kana kwamba ni rangi ya kaharabu, kama kuonekana kwa moto ndani yake pande zote, tangu kuonekana kwa viuno vyake na juu; na tangu kuonekana kwa viuno vyake na chini, niliona kana kwamba ni kuonekana kwa moto; tena palikuwa na mwangaza pande zake zote.


Kama kuonekana kwa upinde wa mvua, ulio katika mawingu siku ya mvua, ndivyo kulivyokuwa kuonekana kwa mwangaza ule pande zote. Ndivyo kulivyokuwa kuonekana kwake mfano huo wa utukufu wa BWANA. Nami nilipoona nilianguka kifudifudi, nikasikia sauti ya mmoja anenaye.


Ni nani awezaye kusimama mbele za ghadhabu yake, naye ni nani awezaye kukaa katika ukali wa hasira yake? Hasira yake kali humwagwa kama moto, nayo majabali yapasuliwa na yeye.


kwa kuwa BWANA, Mungu wenu, ni moto uangamizao, Mungu mwenye wivu.


Kutoka mbinguni amekufanya usikie sauti yake, ili akufundishe; na juu ya nchi alikuonesha moto wake mkuu; ukasikia maneno yake kutoka katika moto.


Basi jua siku hii ya leo kuwa BWANA, Mungu wako, ndiye atanguliaye kuvuka mbele yako kama moto uteketezao; atawaangamiza, tena atawaangusha mbele yako; ndivyo utakapowafukuza na kuwapoteza upesi, kama alivyokuambia BWANA.


Maana hamkufikia mlima uwezao kuguswa, uliowaka moto, wala wingu jeusi, na giza, na tufani,


maana Mungu wetu ni moto ulao.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo