Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Kutoka 23:9 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

9 Usimwonee mgeni; maana, ninyi mwajua moyo wa mgeni ulivyo, kwa kuwa ninyi mlikuwa wageni katika nchi ya Misri.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

9 “Usimdhulumu mgeni; nyinyi mwajua hali ya kuwa mgeni, maana mlikuwa wageni nchini Misri.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

9 “Usimdhulumu mgeni; nyinyi mwajua hali ya kuwa mgeni, maana mlikuwa wageni nchini Misri.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

9 “Usimdhulumu mgeni; nyinyi mwajua hali ya kuwa mgeni, maana mlikuwa wageni nchini Misri.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

9 “Usimdhulumu mgeni; ninyi wenyewe mnajua jinsi mgeni anavyojisikia, kwa sababu mlikuwa wageni Misri.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

9 “Usimwonee mgeni; ninyi wenyewe mnajua jinsi mgeni anavyojisikia, kwa sababu mlikuwa wageni Misri.

Tazama sura Nakili




Kutoka 23:9
13 Marejeleo ya Msalaba  

Wanamwua mjane na mgeni; Wanawaua yatima.


Lakini akipona siku moja au mbili hataadhibiwa; maana, ni mali yake.


Mtu atakayemchinjia sadaka mungu yeyote, isipokuwa ni yeye BWANA peke yake, na angamizwe kabisa.


Usimwonee mgeni, wala kumtendea jeuri; kwa kuwa ninyi mlikuwa wageni katika nchi ya Misri.


Watu wa nchi wametumia udhalimu, wamenyang'anya kwa nguvu; naam, wamewatenda jeuri maskini na wahitaji, nao wamewaonea wageni bila haki.


Ndani yako wamedharau baba na mama; kati yako wamewatenda wageni udhalimu; ndani yako wamewaonea yatima na mjane.


Na mgeni akikaa pamoja nawe katika nchi yako, usimdhulumu.


nawe, je! Haikukupasa kumrehemu mtumwa mwenzako, kama mimi nilivyokurehemu wewe?


Basi, mpendeni mgeni, kwa sababu ninyi wenyewe mlikuwa wageni katika nchi ya Misri.


Usimchukie Mwedomi; kwa kuwa ni ndugu yako; usimchukie Mmisri, kwa kuwa ulikuwa mgeni katika nchi yake.


Na alaaniwe apotoaye hukumu ya mgeni, na yatima, na mjane aliyefiliwa na mumewe. Na watu wote waseme, Amina.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo