Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Kutoka 23:26 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

26 Hapatakuwa na mwenye kuharibu mimba, wala aliye tasa, katika nchi yako; na hesabu ya siku zako nitaitimiza.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

26 Hakutakuwa na mwanamke yeyote atakayepoteza mimba wala kuwa tasa katika nchi yenu. Nami nitawajalia maisha marefu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

26 Hakutakuwa na mwanamke yeyote atakayepoteza mimba wala kuwa tasa katika nchi yenu. Nami nitawajalia maisha marefu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

26 Hakutakuwa na mwanamke yeyote atakayepoteza mimba wala kuwa tasa katika nchi yenu. Nami nitawajalia maisha marefu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

26 na hakuna atakayeharibu mimba wala atakayekuwa tasa katika nchi yako. Nami nitakupa maisha makamilifu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

26 na hakuna atakayeharibu mimba wala atakayekuwa tasa katika nchi yako. Nami nitakupa maisha makamilifu.

Tazama sura Nakili




Kutoka 23:26
16 Marejeleo ya Msalaba  

Abrahamu akafariki, naye akafa katika uzee mwema, mzee sana, ameshiba siku, akakusanyika kwa watu wake.


Naye Isaka akakata roho, akafa, akakusanyika kwa watu wake, ni mzee, ameshiba siku. Esau na Yakobo, wanawe, wakamzika.


Basi Daudi alipokuwa mzee kwa kuishi siku nyingi; alimtawaza mwanawe Sulemani awe mfalme wa Waisraeli.


Fahali wao huvyaza wala hapungukiwi na nguvu; Ng'ombe wao jike huzaa, asiharibu mimba.


Basi Ayubu akafa, akiwa mzee sana mwenye kujawa na siku.


Utafika kaburini mwenye umri mtimilifu, Kama mganda wa ngano ulivyo wakati wake.


Naye aliwabariki wakaongezeka sana, Wala hawapunguzi mifugo wao.


Ghala zetu na zijae Zenye akiba za jinsi zote. Kondoo zetu na wazae Elfu na makumi elfu mashambani mwetu.


Nawe, Ee Mungu, utawateremsha, Wafikie shimo la uharibifu; Watu wa damu na hila hawataishi nusu ya siku zao, Bali mimi nitakutumaini Wewe.


Miaka ya maisha yetu ni sabini, Na ikiwa tuna nguvu miaka themanini; Tena kiburi chake ni taabu na ubatili, Maana wakati unapita upesi nasi kutokomea punde.


Hatakuwapo tena mtoto wa siku chache, wala mzee asiyetimia siku zake; kwa maana mtoto atakufa mwenye umri wa miaka mia; bali mtenda dhambi mwenye umri wa miaka mia atalaaniwa.


Wape, Ee BWANA; utawapa kitu gani? Wape tumbo lenye kuharibu mimba na maziwa makavu.


Utabarikiwa uzao wa tumbo lako, na uzao wa nchi yako, na uzao wa wanyama wako wa mifugo, kuongezeka kwa ng'ombe wako, na wadogo wa kondoo wako.


Basi, zishike sheria zake, na amri zake, ninazokuamuru leo, upate kufanikiwa, wewe na watoto wako baada yako, na siku zako ziwe nyingi katika nchi ile akupayo BWANA, Mungu wako, milele.


Utabarikiwa kuliko mataifa yote; hakutakuwa na mwanamume wala mwanamke aliye tasa kati yenu; wala kati ya wanyama wenu wa kufugwa.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo